JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD NA MSHIRIKA WAKE AIR SERBIA WASAIDIA WAKIMBIZI NA YATIMA WA BELGRADE

Share This
 Kutoka Kushoto ni Rais wa Kamati ya Bunge, Mwakilishi kutoka WAHA na Balozi wa Falme za Kiarabu-Serbia wakikabidhi msaada kwa watoto mjini Bulgade.

 Wawakilishi kutoka Serikali ya Serbia, Shirika la Etihad, Shirika la Serbia, WAHA na Ubalozi wa Falme za Kiarabu- Serbia wakiwa na watoto.

SHIRIKA la ndege la Etihad na mshirika wake, Air Serbia  yamesaidia vifaa vya kukinga baridi, pamoja na vifaa vya shule ikiwamo mabegi  ya shule na vyakula  kwa watoto wakimbizi zaidi ya 2,000 na yatima mjini Belgrade.  

Misaada hiyo ambayo ilikabidhiwa rasmi katika kituo cha Krnjaca Asylum kilichopo mji mkuu wa Serbia, ni mwendelezo wa mpango wa kidunia wa kusaidia elimu na jamii ulioanzishwa na mashirika ya Ndege ya Umoja wa Falme za Kiarabu. Watoto katika kituo hicho waliungana na watoto yatima kutoka jumba la watoto na vijana, hivyo kupata wasaa wa kusherehekea pamoja nao. 

Tukio hilo lililoongozwa na mtangazaji maarufu wa runinga, Minja Subota lilipambwa na nyimbo za kwaya kutoka kwa watoto wa Serbia, vichekesho na mazingaombwe pamoja na kikundi cha wasanii wa jadi na waimbaji maarufu kutoka Serbia kama vile Talija na Zeljiko Vasic.

Aidha, wakati wa tukio hilo, wawakilishi wa Etihad walitembelea kituoni hapo, hususani katika jumba la watoto na vijana lililopo Sremcica Septemba mwaka huu,  huku wakitumia muda wao na watoto pamoja na wafanyakazi sambamba na uchangiaji wa makoti ya kujikinga baridi, mablanketi na baiskeli za walemavu. 

Tukio hilo ni sehemu ya makubaliano kati ya Shirika la Etihad na Ubalozi wa Falme za Kiarabu mjini Belgrade katika kutoa misaada ya kibinadamu na kusaidia jamii nchini Serbia. Katika kipindi cha miaka minne iliyopita, Shirika la Etihad pia lilitoa misaada ya kielimu kwa watoto wa Yemen, Morocco, Sri Lanka, Kenya na Jordan.

Rais wa Kamati ya Bunge nchini Serbia, Maja agojkovic alilishukuru Shirika la Etihad na Shirika la Serbia pamoja na washiriki wao kwa msaada huo, hususan katika kusaidia vifaa vya elimu na vifaa vya shule hasa katika kipindi hiki cha kuanza mwaka mpya wa masomo.

Makamu Mkuu wa Rais wa Viwanja vya Ndege vya Abudhabi, Khaled Al Mahairbi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo na Jamii alisema: “Kila mtoto anatakiwa kuishi katika mazingira rafiki na yenye usalama pamoja na upatikanaji wa elimu. Inasikitisha kuona mambo haya mara kwa mara hayawezekani katika dunia hii, hivyo tunatarajia kwamba juhudi hizi kwa namna fulani zitawasaidia watoto hawa kwa miezi ijayo. Shukrani zetu za pekee ziwaendee UNHCR kwa kutuunga mkono katika kurudisha nyuso za furaha kwa watoto.

 Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Serbia, Mheshimiwa Juma Rashidi Aldhaheri alisema, “Ninawashukuru Etihad, Shirika la Serbia, WAHA pamoja na washirika wetu wote kwa juhudi zao katika harakati hizi, hii inaonyesha kwamba taasisi nyingi pamoja na mataifa yanaweza kufanya kazi pamoja ili kusaidia wenye uhitaji.”

Naye Mtendaji Mkuu wa Shirika la Serbia Dane Kondich alisema, “Tunafurahi  kuwa sehemu ya juhudi hizi pamoja na washirika wetu katika Serikali ya Serbia na Shirika la Etihad ili kuwaonesha watoto hawa kwamba watu wanawajali siyo tu leo, bali hata katika wiki na Miezi ijayo.”

Mwakilishi wa Rais kutoka Taasisi ya Kimataifa ya WAHA (The Women and Health Alliance International) Dr. Khawla Salem Rashed Al Saaedi aliongeza kwamba “Ni furaha kubwa  na utukufu kwangu kuhudhuria  tukio hili la kipekee ambalo lina maana ya muungano mpya  kati ya washirika wote. Natarajia kuwa tukio hili litakuwa nyenzo ya matumaini kwa watoto hawa vilevile ni mfano wa kuigwa kwa wanaotaka kuonesha utu wao katika kuwasaidia wenye uhitaji.

Katika tukio hilo, kulikuwa na hotuba maalumu kutoka kwa Waziri wa Kazi, Ajira , wastaafu na mambo ya kijamii  kutoka Jamhuri ya Serbia Bwana Aleksandar Vulin, Waziri wa Elimu, Sayansi na Maendeleo ya Tekinolojia; Mladen Sarcevic, Rais wa Bunge la Serbia, Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo na Jamii ya Etihad, Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Serbia, mwakilishi kutoka WAHA na Mtendaji mkuu wa Shirika la Serbia.

Tukio hilo pia lilihudhuriwa na Makamu wa Rais- Mikakati kwa Wazawa Bw. Ali Al Shamsi, Makamu wa Rais – Huduma za Wageni  (wote kutoka Etihad); pia  Afisa Mkuu wa Serikari na Mwenyekiti wa  wadau wa Shirika (wote kutoka Shirika la Serbia).

Msaada uliotolewa mjini Bulgrade umetokana na Fedha zilizochangishwa kupitia mfululizo wa Harambee zilizo fanyika Abu Dhabi kwa kushirikiana na Taasisi ya WAHA. Miongoni mwa harambee hizo zinajulikana kama ‘Walk For a Cause’ Uuzwaji  wa Karakana ya Etihad na Mashindano ya mpira wa miguu ya Mwezi wa Ramadhani. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad