JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LASHEREKEA SIKUKUU YA ‘CHUSEOK’ NA WAKOREA NCHINI TANZANIA

Share This
 Kutoka kushoto, Grace Kijo- Mratibu wa Masoko wa Etihad nchini Tanzania na Balozi wa Korea nchini Tanzania, Song Geum –Young, wakimpongeza Bi. Heejin Hwang (kulia) kwa kushinda moja ya tiketi tatu za safari ya Korea. Washindi wengine wawili katika sherehe hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam ni YoungMi Choi na Sunmi Oh
 .Kutoka kushoto; Grace Kijo, Balozi wa Korea na Bi. HaeMyung Rhee, Mwenyekiti wa Chama cha Korea, wakimpongeza Bi. Heejin Hwang. kwa kushinda moja ya tiketi tatu za safari ya Korea. Washindi wengine wawili katika sherehe hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam ni YoungMi Choi na Sunmi Oh.
Grace Kijo akipokea tuzo ya kutambua mchango wa Shirika hilo kwa niaba ya Etihad.

SHIRIKA la Ndege la Etihad lenye makao makuu yake Nchi za Falme za Kiarabu limeungana na Jumuiya ya Wakorea waishio nchini Tanzania kuadhimisha sherehe ya kitamaduni ya taifa hilo inayofahamika kama ‘CHUSEOK’ kwa kutoa tiketi kwa safari watatu kutoka Dar es Salaam kwenda Incheon-South Korea.

Akizungumza katika hotuba yake, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya Wakorea wanaoishi hapa nchini, Bi. Hae Myung Rhee alilishukuru Shirika la Ndege la Etihad kwa udhamini wake kwenye sherehe hizo zilizohudhuriwa na wageni waalikwa na wadau muhimu pamoja na wafanyabiashara na wanachama takribani 250 wa jamii ya Kikorea hapa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad