JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LASAIDIA KITUO CHA MICHEZO SOKOINE JOGGING CLUB TANZANIA

Share This
 Watoto wa kituo cha michezo cha Sokoine jogging club Tanzania kilichopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kushiriki michezo ya kirafiki kwa udhamini wa Shirika la ndege la Etihad iliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.
 Mwanafunzi kutoka shule ya Msingi Madenge iliyopo Temeke jijini Dar es salaam Mselemu Omary akigombania mpira na Sultan Said wa Shule ya Msingi Kibasila katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika Uwanja wa Taifa wa Uhuru mwishoni mwa juma.
 Mratibu wa Masoko wa Shirika la Ndege la Etihad Tanzania, Grace Kijo akigawa viburudisho kwa watoto wa kituo cha michezo cha Sokoine jogging club Tanzania kilichopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam,mara baada ya watoto hao kushiriki michezo ya kirafiki iliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.
Afisa Mauzo wa Shirika la Ndege la Etihad Tanzania, Bhavin Sonegra akigawa keki kwa watoto wa kituo cha michezo cha Sokoine jogging club Tanzania kilichopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam,mara baada ya watoto hao kushiriki michezo ya kirafiki iliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.

Shirika la Ndege la Etihad lenye makao yake makuu katika nchi za Falme za Kiarabu mwishoni mwa wiki iliyopita lilimesaidia Kituo cha michezo cha Sokoine jogging club Tanzania kilichopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, hapa nchini.

Shirika hilo lililojinyakulia tuzo tatu za ubora wa huduma za anga kwa mwaka huu, limetoa vifaa vya shule na michezo pamoja na viburudisho mbalimbali baada ya watoto wa kituo cha michezo cha Sokoine kushiriki mechi ya kirafiki na michezo mbalimbali iliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, jijini Dar es salaam.

Zaidi ya watoto 90 wa kituo hicho wengi wao kuanzia umri kati ya miaka 10-14 walijumuika kushiriki michezo  hiyo ya kirafiki iliyohusisha michezo ya mpira wa miguu kwa wavulana na netiboli kwa wasichana.

Bonanza hilo lililenga kuimarisha umoja na afya kwa vijana. Kituo cha Michezo cha Sokoine jogging club kilianzishwa 20 Agosti, 2014 kwa lengo la kusaidia vijana wa umri wa miaka 7-15 kunufaika kwa kupitia michezo na mazoezi ya kukimbia ( jogging).

Akilishukuru Shirika la Ndege la Etihad, mwanzilishi wa kituo hicho cha michezo, Bwana Felix Kauta Massawe (38) alisema,” Tunashukuru sana kwa kupokea msaada huu mkubwa kutoka Shirika la Ndege la Etihad. Vifaa hivi vitatusaidia kwenye shughuli zetu za kila siku hapa kituoni.”

 “Kituo chetu cha michezo kina takriban wanafunzi 120 ambao wanahitaji vifaa muhimu kwenye mafunzo tunayowapa, hili siyo tu tunawasaidia kupata elimu ya michezo bali pia inawaimarisha kiafya kupitia michezo na mazoezi wanayopata."

Mratibu wa Masoko wa Shirika la Ndege la Etihad nchini, Grace Kijo alisema, “Tunaamini kwamba kwa kuwasaidia vijana hawa tunaandaa taifa la vijana wenye nguvu na afya huku dhumuni lete likiwa kudhamini zaidi kwenye vituo vya michezo na matukio mengine kama haya kwa siku za karibuni.”

 “Shirika la Ndege la Etihad limedhamiria kusaidia na kuleta mabadiliko kwenye jamii ambako linafanya shughuli zake. Mchango wetu wa dhati wa shirikia hili ni kuhakikisha linasaidia juhudi zilizoanzishwa za kuleta maendeleo endelevu kwenye jamii na kuboresha maisha ya jamii ikiwamo elimu kwa watoto na kuwezesha maisha yao,” alisema Kijo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad