SERIKALI
ya Tanzania imeridhia rasmi utekelezaji wa mradi ujenzi wa bomba la mafuta ghafi
kutoka Kabaale katika Wilaya ya Hoima nchini Uganda hadi bandariya Tanga nchini
Tanzania.
Uamuzi
huo umefikiwa katika Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo (tarehe 29
Septemba, 2016) Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Taarifa
ya kuridhiwa rasmi kwa mradi huo imetolewa naWaziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambaye
amesema ujenzi wa mradi huo utakaoanza wakati wowote kuanzia sasa unatarajiwa kukamilika
mwaka 2020.
Amesema
ujenzi wa bomba hilo unatarajiwa kugharimu dola za Marekani Bilioni 3.5 ambapo kati
yake Dola Bilioni 3 zitatumika kujenga bomba upande wa Tanzania.
Mradi
huom kubwa utatekelezwa kwa ubia wa ujenzi na uendeshaji kwa kushirikishaka mpuni
za Total ya Ufaransa, CNOOC ya China, Tullow ya Uingereza na Serikaliza
Tanzania na Uganda.
Mhe.
Majaliwa ameongeza kuwa bomba hilo lenye urefu wa kilometa 1,443 linatarajiwa kusafirisha
mapipa 200,000 kwa siku ambapo kila pipa litaliingizia taifa Dola za Marekani
12.2.
Amebainisha
kuwa pamoja na kusafirisha mafuta ya kutoka nchini Uganda bomba hilo pia linatarajiwa
kusafirisha mafutakutoka nchi nyingine zaJ amhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudani
Kusini ambazo zimeonesha nia ya kusafirisha
mafuta yao kupitia bandari ya Tanga.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa ametaja faida nyingine ambazo Tanzania itazipata kutoka na
namradi huo kuwa ni kupatika na kwa ajira zaidi ya 15,000 wakati wa ujenzi na ajira
2,000 baadaya ujenzi kukamilika, kuimarika kwa mahusiano ya kidiplomasia,
kukuza biashara katika ukanda wa kaskazini mwa Tanzania, kampuni za ujenziza
Tanzania kupata kazi za ujenzi.
Aidha,
amesema Tanzania inatarajia kunufaika zaidi kwa kutumia bomba hilo kupitisha mafuta
yanayotarajiwa kupatikana katika maeneo ya ziwa Tanganyika na Ziwa Eyasi
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATANO, SEPTEMBA 28, 2016
0 comments:
Post a Comment