728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, September 20, 2016

  SERIKALI KUSAMBAZA CHAKULA SALAMA KWA WAATHIRIKA WA SUMUKUVU

  Naibu Waziri Wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigangwala akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari na watafiti mbalimbali hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa mkutano wa watafiti wa chakula uliojadili madhara na athari za sumukuvu uliofanyika jijini Dar es salaam.
  Naibu Waziri Wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigangwala wa kwanza kulia akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu Bw. Hiiti Silo kushoto na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma na ubora Wizara ya afya Dkt. Mohammed Mohammed katikati wakati wa uzinduzi wa mkutano wa watafiti wa chakula uliojadili madhara na athari za sumukuvu uliofanyika jijini Dar es salaam.
  Watalaamu wa utafiti na wadau mbalimbali wa afya kutoka nchi mbalimbali wakifuatilia kwa makini maelezo ya Naibu Waziri Wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigangwala hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa mkutano wa watafiti wa chakula uliojadili madhara na athari za sumukuvu uliofanyika jijini Dar es salaam.

  Picha zote Na Ally Daud-Maelezo

  ………………………………………………….

  Na Ally Daud-Maelezo

  SERIKALI imesambaza chakula salama na kutoa tiba bure kwa waathirika wa ugonjwa wa mlipuko wa sumukuvu katika mikoa ya Dodoma na Manyara uliotokea hivi karibuni.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri Wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigangwala wakati wa uzinduzi wa mkutano wa watafiti wa chakula uliojadili madhara na athari za sumukuvu.

  Dkt. Kigwangala alisema Serikali imeandaa utaratibu wa kuwapelekea vyakula salama waathirika wa ugonjwa huo na kuteketeza vyakula vyenye sumukuvu.

  “Tumepanga utaratibu wa kupeleka vyakula salama kwa waathirika wa ugonjwa a sumukuvu katika mikoa husika bila malipo ili kusaidia kuondoa ugonjwa huo na kuteketeza mabaki ya vyakula vyenye vizaria vya sumukuvu” alisema Dkt. Kigangwala

  Aidha Dkt. Kigwangala alisema kuwa Serikali ipo bega kwa bega na waathirika wa sumukuvu ili kuhakikisha wanaondoa ugonjwa huo kwani tayari umethibitishwa na wataalamu na unapatikana kwenye mazao ya vyakula kama vile mahindi, uwele, mtama na karanga.

  Kwa mujibu wa Dkt. Kigangwala alisema katika kukabiliana na ugonjwa huo Serikali imeamua kushirikiana na wataalamu wa kimataifa ili kuweza kuondoa ugonjwa huo kwenye vyakula vinavyolimwa nchini ili kuyawezesha mazao mazao hayo kuuzwa kwa urahisi hapa nchini.

  Dkt Kigwangala aliwashukuru watafiti hao kwa kugundua chanzo cha ugonjwa huo ambao unasababishwa na Jamii ya fangasi wanaoitwa Aspergillus wanaojikita zaidi kwenye vyakula na kuwataka wapate matokeo chanya ya kutokomeza sumukuvu.

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Silo alisema katika mkutano huo watafiti hao wanatarajia kujadili na kupata ufumbuzi wa tafiti za vyakula mbalimbali ili visiendelee kuleta madhara kwa Watanzania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SERIKALI KUSAMBAZA CHAKULA SALAMA KWA WAATHIRIKA WA SUMUKUVU Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top