728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, September 19, 2016

  SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA MAENDELEO NCHINI.

   Kikundi cha wahitimu wa elimu ya juu SUJA ECO-ENERGY wakiwa na mfano wa hundi ya dola 3000 ambayo wamekabidhiwa baada ya kubuni wazo la kijasiriamali la mradi wa kutengeneza nishati kupitia kinyesi cha ng’ombe.
   Kikundi cha wahitimu wa elimu ya juu cha RECHA wakikabidhiwa mfano wa hundi ya dola 3000 kutoka kwa Mkurugenzi wa Teknolojia na Operesheni  wa Benki ya Posta Tanzania Bw.Jema Msuya . Benki ya Posta Tanzania ni moja ya waliodhamini mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wahitimu wa elimu ya juu.
  Kikundi cha wahitimu wa elimu ya juu cha GBL Bucket Toilet Co. wakiwa katika picha ya pamoja na mwakilishi kutoka mfuko wa ubunifu wa maendeleo kwa binadamu (HDIF)Bw. David McGinty baada ya kujishindia dola 3000.Wahitimu hao wameshinda pesa izo baada ya kubuni mradi wa kutengeneza choo ambacho kinatumia ndoo ya plastic
  Na Daudi Manongi,MAELEZO
   Bi Mwaka Miyeye (kushoto) akitoa maelezo kwa mmoja ya watu waliotembelea kuona moja ya mradi walibuni baada ya kumaliza mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wahitimu wa elimu ya juu nchini.
   Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Taasisi ya Kifedha ya UTT-Microfinance Bw.James Washima akifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi(hayupo Pichani) wakati mgeni uyo akifunga mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wahitimu wa elimu ya juu nchini.Pembeni  yake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea Bi.Haigath Kitala.(katikati)
   Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya waziri mkuu Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira na Vijana Bw.James Kajugusi akizungumza  katika kilele cha mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wahitimu wa elimu ya juu nchini yaliyofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.


  Na Daudi Manongi- MAELEZO ,Dar es Salaam 

  Serikali kupitia Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi limesema kuwa litaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo nchini ili kutatua changamoto ya ajira kwa vijana. 

  Hayo yamesemwa juzi Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Vijana katika Ofisi ya Waziri Mkuu, James Kajugusi wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wahitimu wa elimu ya juu nchini. 

  “Uwezeshaji wananchi kiuchumi ni dhana pana inayohitaji ushirikiano wa karibu kati ya serikali na sekta binafsi pamoja na wadau wa maendeleo na katika kuchochea juhudi za uwezeshaji wananchi kiuchumi” alisemaBw.Kajugusi 

  Akizungumzia kuhusu changamoto zinazowakabili vijana nchini, Kajugusi alisema kuwa changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana imechochewa na mabadiliko ya kisera na kiuchumi yanayosimamiwa kwa dhati na serikali katika kupeleka mbele zaidi taifa letu katika nyanja za kijamii na kiuchumi. 

  Awali akizungumza na vijana 22 waliohitimu mafunzo hayo aliwataka vijana hao kuongeza ari ya kufanya kazi na kushiriki fursa mbalimbali zinazojitokeza zenye lengo la kujikwamua kiuchumi. 

  “Vijana mtumie vema fursa mbalimbali za uwezeshaji mnazozipata kwa kuboresha zaidi uelewa wenu na hali zenu za maisha” Alisema Kajugusi 

  Kwa upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi, Bi Anna Mtaita amesema kuwa Baraza hilo litaendelea kuthamini nchini na kwa kulitambua hilo maana wameamua kushirikiana na taasisi ya maendeleo ya Cambridge katika kuratibu na kutoa mafunzo hayo. 

  Mtaita aliongeza kuwa mbali na programu hiyo, Baraza hilo pia linaratibu programu ya majaribio kwa vijana walio katika mazingira magumu katika kuwapatia mafunzo, malezi, na kuwaunganisha na mitaji. 

  Kwa mujibu wa Mtaita alisema mpaka kufikia sasa Baraza hilo limewawezesha vijana 500 nchini katika upataji wa mafunzo, malezi na mitaji. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA MAENDELEO NCHINI. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top