728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, September 18, 2016

  SERENGETI BOYS YAIKUNA CONGO BRAZZAVILLE 3-2 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR LEO

  Mpaka dakika 90 za mchezo.

  TIMU ya Serengeti Boys imefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Congo Brazaville katika mchezo wa kufuzu kuingia fainali za mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 nchini Madagascar  uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa.

  Katika mchezo huo ulioanza kwa kasi na kila upande kushambuliana kwa zamu zilianza kuzaa matunda kwa timu ya Serengeti Boys kuandika goli la kwanza dakika ya 38 liliolofungwa na Yohana Mkomola na dakika ya 42 akafanikiwa kuongeza goli la pili kwa Serengeti Boys.

  Mpaka inafikia mapumziko Serengeti Boys walikuwa mbele kwa goli 2-0 lakini dakika ya 73, Langa-Lesse Percy anaiandikia Congo Brazzaville goli la kwanza kwa mkwaju wa penati baada mchezaji kuangushwa ndani ya eneo la hatari.

  Issa Makamba anaipatia Serengeti Boys goli la tatu akitumia nafasi nzuri aliyoipata lakini halikudumu sana katika dakika ya 90 Poboumela Chardon akaipatia Congo Brazzaville goli la pili kwa kutumia uzembe wa goli kipa Kelvin Kayego aliyeingia kuchukia nafasi ya Ramadhan Kabwili aliyeumia wakati akiokoa penati.

  Mpaka mpira unamalizika Serengeti Boys wametoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 3-2.

  Kila timu iliweza kufanga mabadiliko na kwa upande wa Serengeti Boys walimtoaYohana Mkomola na kuingia Issa Makamba, Ibrahim Ali na kuingia Muhsin Makame na kwa Congo Brazaville alitoka Mboungou Prestige na kuingia Mountou Edoward, Mantourari Aldo na kuingia Makoina Beni na Kiba Konde Rodrique na kuingia Bopoumela Chardon.
  Mnamo kipindi cha pili mchezaji wa timu ya Serengeti Boys,Issa Abdi Makamba anaipatia goli la 3 dhidi ya timu ya Congo Brazzaville.Mpaka mpaka dakika 90 za mchezo,timu ya Serengeti Boys wameibuka washindi kwa kuiburuza timu ya Congo Brazzavile 3-2 ,uwanja wa Taifa jijini Dar.

  Timu ya Serengeti Boys (Tanzania),katika kipindi cha kwanza ilikuwa ikiongoza  goli 2-0 ,ambapo mnamo dakika ya 40 na 42 mchezaji Yohana Oscar Mkomola aliipatia timu yake magoli mawili dhidi ya timu ya Congo Brazaville,katika mchezo unaonendelea hivi sasa katika uwanja wa Taifa jijini Dar,ambapo Brazzaville wamejipatia goli la pili kipindi cha pili.Serengeti boys wameifunga Congo Brazzavile goli 3-2 dhidi ya Congo Brazzavile,goli la tatu limefungw na mchezaji Issa Abdi Makamba.Mchezaji wa timu ya Serengeti Boys,Yohana Oscar Mkomola akitoka mbio maara baada ya kuachia mkwaju mkali kwa golikipa wa timu ya Congo Brazaville,na kutinga wavuni,likiwa ni goli la pili mnamo dakika ya 42 kipindi cha kwanza.MPaka sasa Serengeti boys wanaongoza goli 3-2 dhidi ya timu ya Congo Brazzaville,katika mchezo unaondelea hivi sasa,uwanja wa Taifa jijini Dar.
  Mashabiki wakimshangilia mchezaji wa timu ya Serengeti Boys,Yohana Oscar Mkomola mara baada ya kufungua goli la pili dhidi ya timu ya Congo Brazzaville.


  Mchezaji wa timu ya Congo Brazzaville Ngumbi Exau akiruka hewani kumzuia mchezaji wa timu ya Serengeti Boys Yohana Oscar Mkomola asiondoke na mpira.
  Katika kipindi cha kwanza kila timu ilionesha kiu kubwa ya kutaka kupata magoli mapema,kila timu ilikuwa ikishambulia lango la mwenzake kwa spidi kubwa,mpaka dakika 90 za mchezo timu ya Srengeti Boys imeibuka kwa ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Congo Brazzavile.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAIKUNA CONGO BRAZZAVILLE 3-2 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR LEO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top