728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, September 18, 2016

  SERENGETI BOYS INAONGOZA 2-1 DHIDI YA CONGO BRAZZAVILLE MPAKA SASA


  Timu ya Serengeti Boys (Tanzania),katika kipindi cha kwanza ilikuwa ikiongoza  goli 2-0 ,ambapo mnamo dakika ya 40 na 42 mchezaji Yohana Oscar Mkomola aliipatia timu yake magoli mawili dhidi ya timu ya Congo Brazaville,katika mchezo unaonendelea hivi sasa katika uwanja wa Taifa jijini Dar,ambapo Brazzaville wamejipatia goli la kwanza kipindi cha pili na mpira unaendelea.Mchezaji wa timu ya Serengeti Boys,Yohana Oscar Mkomola akitoka mbio maara baada ya kuachia mkwaju mkali kwa golikipa wa timu ya Congo Brazaville,na kutinga wavuni,likiwa ni goli la pili mnamo dakika ya 42 kipindi cha kwanza.MPaka sasa Serengeti boys wanaongoza goli 2-1 dhidi ya timu ya Congo Brazaville,katika mchezo unaondelea hivi sasa,uwanja wa Taifa jijini Dar.
  Mashabiki wakimshangilia mchezaji wa timu ya Serengeti Boys,Yohana Oscar Mkomola mara baada ya kufungua goli la pili dhidi ya timu ya Congo Brazaville.


  Mchezaji wa timu ya Congo Brazzaville Ngumbi Exau akiruka hewani kumzuia mchezaji wa timu ya Serengeti Boys Yohana Oscar Mkomola asiondoke na mpira.
  Katika kipindi cha kwanza kila timu ilionesha kiu kubwa ya kutaka kupata magoli mapema,kila timu ilikuwa ikishambulia lango la mwenzake kwa spidi kubwa,mpaka sasa timu ya Srengeti Boys iko mbele goli 2-1 dhidi ya Congo Brazzavile.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS INAONGOZA 2-1 DHIDI YA CONGO BRAZZAVILLE MPAKA SASA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top