728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, September 21, 2016

  RC KILIMANJARO SAID MECK SADICK ATEMBELEA KIWANDA CHA TANGAWIZI

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick akipokea maelezo kuhusu mashine hizo .

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wake wa kazi alipozuru wilaya ya Same


  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
  Said Meck Sadick akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Wilaya ya Same kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki

  Wananchi wakisikiliza kwa makini mkutano wa mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro


  Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki akitoa salamu kwa wajumbe wa kamati ya ulizni na usalama na salamu za kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
  Said Meck Sadick alipotembelea Wilayani hapo

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
  Said Meck Sadick akikagua mashine katika kiwanda cha Tangawizi kilichopo kata ya Miyamba Wilayani Same
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
  Said Meck Sadick alipokagua mfereji wa Mshana


  Na Mathias Canal, Kilimanjaro

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
  Said Meck Sadick amezuru katika kiwanda cha Tangawizi kilichopo kata ya Miyamba Wilayani Same.

  Sadiki ametembelea kiwandani hapo akiwa na dhamira ya kukifufua kiwanda hicho ili kianze kufanya kazi ya izalishaji katika kiwango cha juu ili kwenda sawia na kasi ya Maendeleo inayohitaji kwa wananchi wa eneo hilo sambamba na Taifa kwa ujumla.

  Akizungumza na wananchi kwenye Mkutano wa hadhara alisema kuwa uongozi wa kiwanda hicho pia unapaswa kutunza vyanzo vya maji lakini pia kuchemsha maji ya kunywa ili kuepukana na Maradhi mbalimbali yatokanayo na unywaji wa maji yasiyo safi na salama.

  Katika sekta ya elimu amesema kuwa ni dhahiri kuwa miundombinu ya shule inapaswa kuboreshwa ili waalimu wakae kwenye vituo wanavyopangiwa na kuachana na tabia ya kuhamahama.

  Rc Sadick amezungumzia pia mimba za utotoni ambapo amewataka wananchi kuwaacha watoto wa kike waweze kusoma ili baadae wasiwe tegemezi tofauti na ilivyo sasa anbapo wazazi wengi wanawaozesha wabinti wakiwa na umri mdogo jambo ambalo ni kinyume kabisa na utaratibu wa ndoa kwa mujibu wa sheria ya ndoa.

  Kabla ya mkutano huo Mkuu huyo wa Mkoa wa Kilimanjaro
  Said Meck Sadick, Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same walifanya mazungumzo na Bodi ya uongozi wa Ushirika wa kiwanda hicho na kuwataka waongeze juhudi kuhakikisha wakulima wa Tangawizi hawapati hasara tena.

  Rc Sadick ameutaka uongozi wa viwanda vidogo vidogo SIDO ambao ndio wenye mitambo iliyofungwa kiwandani hapo kuboresha mashine hizo ambazo kwa sasa zinatumia OIL chafu kuhamia kwenye umeme ili kiwanda kiwe rafiki kwa mazingira pia.

  Zao la Tangawizi linalimwa sana katika Kata hiyo ya Miyamba hivyo kufufuliwa kwa kiwanda hicho kutaleta mapinduzi makubwa katika uchumi wa mwananchi mmoja mmoja pamoja na kuongeza ajira kwa wakazi wa maeneo hayo na Taifa kwa ujumla.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: RC KILIMANJARO SAID MECK SADICK ATEMBELEA KIWANDA CHA TANGAWIZI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top