728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, September 30, 2016

  RAIS WA SHIRIKA LA ENGENDER HEALTH LA MAREKANI AKUTANA NA WAZIRI WA AFYA WA ZANZIBAR

   Rais wa Shirika la Engender Health la Marekani Ulla Muller ambae pia ni Mtendaji Mkuu (CEO) wa Shirika hilo akizungumza na Waziri wa Afya  Mahmoud Thabit Kombo alipomtembelea Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar, (kulia) ni Mkurugenzi Ufundi ambae ni Naibu mwakilishi wa Shirika hilo Tanzania Feddy Mwanga.
  afi2
  Maafisa waliofuatana na Rais wa Shirika la Engender Health kutoka Ofisi ya Dar es salaam wakifuatilia mazungumzo ya viongozi hao yaliyofanyika Ofisi ya Waziri wa Afya Mnazimmoja Zanzibar.
  afi3
  Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akiahidi mashirikiano ya karibu na Shirika la Engender Health wakati wa mazungumzo yake na Rais na Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo Ulla Muller Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
  afi4
  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akiagana na mgeni wake Rais na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Engender Health Ulla Muller baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Waziri Mnazimmoja Zanzibar.
  Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: RAIS WA SHIRIKA LA ENGENDER HEALTH LA MAREKANI AKUTANA NA WAZIRI WA AFYA WA ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top