728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, September 1, 2016

  Rais Magufulia amuapisha Bw. Doto M. James kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 01 Septemba, 2016 amemuapisha Bw. Doto M. James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  Bw. Doto M. James aliteuliwa kushika wadhifa huo jana tarehe 31 Agosti, 2016 na amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Servacius Likwelile ambaye atapangiwa kazi nyingine.

  Kabla ya uteuzi huo, Bw. Doto M. James alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera).

  Hafla ya kuapishwa kwa Bw. Doto M. James imehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
  Aidha, Bw. Doto M. James amekula kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma, zoezi ambalo limeongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda.


  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es salaam
  01 Septemba, 2016


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Doto James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Fedha na Mipango Doto James mara baada ya kuapishwa.PICHA NA IKULU

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Rais Magufulia amuapisha Bw. Doto M. James kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top