728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, September 11, 2016

  Rais Magufuli kuwasili Lusaka Zambia kesho kwa ziara ya siku tatu

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho tarehe 12 Septemba, 2016 anatarajiwa kuwasili Mjini Lusaka nchini Zambia kwa ziara ya siku tatu ambapo pamoja na mambo mengine atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu zitakazofanyika keshokutwa tarehe 13 Septemba, 2016 katika Jiji la Lusaka.

  Rais Magufuli anafanya ziara hii ya kwanza nchini Zambia akiwa pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa,Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

  Kamati hiyo inajulikana kwa jina la SADC-Troika.

  Dkt. Magufuli alipokea kijiti cha Uenyekiti wa SADC-Troika kutoka kwa Rais wa nne Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi katika Mkutano wa 36 wa SADC uliofanyika katika Jiji la Mbabane nchini Swaziland tarehe 01 Septemba, 2016.

  Katika Ziara hii Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na Viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika watakaohudhuria sherehe hizo zitakazofanyika katika Uwanja wa Mashujaa Jijini Lusaka.
   
  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Lusaka
  11 Septemba, 2016
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Rais Magufuli kuwasili Lusaka Zambia kesho kwa ziara ya siku tatu Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top