728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, September 6, 2016

  Rais Magufuli atoa siku 7 kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kumaliza deni wanalodaiwa na NHC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipanda kwenye gorofa ya kwanza katika  mojawapo ya mabweni yanayojengwa na Wakala wa Majengo nchini TBA katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mabweni hayo yatakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 3840 kwa wakati mmoja na yatakamilika mwezi wa kumi na mbili.
  mli2
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo kuhusu ujenzi wa mabweni hayo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo(TBA) Arch. Elius Mwakalinga, Mabweni hayo yatakuwa na uwezo wa kuchukua wanafuzi zaidi ya 3840.
  mli3
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo kuhusu ujenzi wa mabweni hayo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Arch. Elius Mwakalinga. Mabweni hayo yatakuwa na uwezo wa kuchukua wanafuzi zaidi ya 3840.
  mli4
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua baadhi ya maeneo katika gorofa ya kwanza ya moja ya mabweni hayo katika eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  mli5
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako wakiangalia kwa furaha maendeleo ya ujenzi wa mabweni hayo unavyoendelea kwa kasi katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaa.
  mli6
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa Mabweni hayo.
  mli7
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza  mara baada ya kukagua ujenzi wa mabweni katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  mli8
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi waojenga mabweni hayo kutoka kwa Wakala wa Majengo nchini TBA. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Elius Mwakalinga, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Joseph Nyamhanga, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Hamfrey Polepole.
  mli9
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi waojenga mabweni hayo kutoka TBA.
  ……………………………………………………………
  Na: Lilian Lundo – MAELEZO
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 7 kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kulipa deni la bilioni 2 ambalo wanadaiwa na Shirika la nyumba la Taifa (NHC).

  Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo kwa Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi, Injinia Joseph Nyamhanga leo jijini Dar es Salaam katika ziara ya kushtukiza ya kuangalia ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  “Nawapa siku 7 muwe mmelilipa hilo deni huku mkiendelea na utaratibu wa kuhamia Dodoma, kama hamtalilipa kwa wakati nitawaagiza NHC kuwatolea vitu vyenu nje kama wanavyofanya kwa wengine,” alisema Dkt. Magufuli.

  Amesema kuwa kiwango hicho cha bilioni 2 kingeiwezesha wizara hiyo kujenga ofisi za wizara kwa kuwatumia Wakala wa Majengo (TBA) ambao wako chini ya wizara hiyo badala ya kutumika kama kodi ya pango.
  Aidha, ameitaka wizara hiyo kuhamia Mjini Dodoma mara tu watakapokamilisha deni hilo na kutoendelea kupanga jijini Dar es Salaam, kwani hakuna sababu ya kuendelea kupanga majengo ya ofisi Dar es Salaam wakati Serikali yote inahamia Dodoma.

  Wakati huohuo, Rais Dkt. Magufuli ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Tecknolojia, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na  Wakala wa Majengo (TBA) na uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kusimamia  vizuri mradi wa ujenzi wa hosteli za chuo kikuu ambao Rais mwenyewe aliahidi shilingi bilioni 10 katika ujenzi huo, bilioni 5 imekwishatolewa na bilioni nyingine 5 itatolewa ndani ya wiki hii.  

  Hosteli hizo zinategemea kuchukua wanafunzi 4000 ambapo itapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la wanafunzi kukaa nje ya maeneo ya chuo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Rais Magufuli atoa siku 7 kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kumaliza deni wanalodaiwa na NHC Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top