728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, September 9, 2016

  Rais Magufuli ateua Makatibu Tawala wa Mikoa ya Rukwa na Mara


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09 Septemba, 2016 amemteua Bw. Ado Steven Mapunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara.

  Bw. Ado Steven Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Benedict Richard Ole Kuyan ambaye amestaafu.

  Pia, Rais Magufuli amemteua Bw. Tixon Tuliangine Nzunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.

  Bw. Tixon Tuliangine Nzunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Symthies Emmanuel Pangisa ambaye amestaafu.

  Tarehe ya kuapishwa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa walioteuliwa itatangazwa baadaye.


  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es Salaam
  09 Septemba, 2016
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Rais Magufuli ateua Makatibu Tawala wa Mikoa ya Rukwa na Mara Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top