728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, September 14, 2016

  Rais Magufuli amwapisha Dkt. Ramadhan Dau kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia na Makatibu Tawala wa Mikoa watatu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Ramadhani Dau kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Ikulu jijini Dar es Salaam.
  dr4
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Tixon Nzunda kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  dr7
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Eliya Ntandu kuwa Katibu Tawala mkoa wa Songwe, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  dr8
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Eliya Ntandu kuwa Katibu Tawala mkoa wa Songwe, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  dr9
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Adoh Mapunda kuwa Katibu Tawala mkoa wa Mara Ikulu jijini Dar es Salaam.
  dr10 dr11
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhani Dau na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba mara baada ya tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  dr12
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Katibu Tawala mkoa wa Mara Bw. Adoh Mapunda wa pili kutoka (kushoto), Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa Bw. Tixon Nzunda watatu kutoka (kushoto) , Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba wapili kutoka (kulia), Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Eliya Ntandu wakwanza (kulia) mara baada ya tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  dr13
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Ramadhani Dau mara baada ya tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  dr14
  Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Ramadhani Dau, Katibu Tawala mkoa wa Rukwa Tixon Nzunda, Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Eliya Ntandu pamoja na Katibu Tawala wa mkoa wa Mara Adoh Mapunda wakila kiapo cha Uadilifu  mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 14 Septemba, 2016 amemuapisha Dkt. Ramadhani Kitwana Dau kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia. 

  Kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi, Dkt. Ramadhan Kitwana Dau alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
  Mhe. Balozi Dkt. Ramadhani Kitwana Dau anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

  Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amewaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa mitatu aliowateua mwishoni mwa wiki iliyopita.
  Walioapishwa ni  kwanza, Bw. Eliya Mtinangi Ntandu anayekuwa Katibu Tawala wa kwanza wa Mkoa wa Songwe ulioanzishwa rasmi Mwezi Februari 2016.

  Pili, Bw. Adoh Stephen Mapunda anayekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara.
  Bw. Adoh Stephen Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Benedict Richard Ole Kuyan ambaye amestaafu.

  Tatu, Bw. Tixon Tuliangine Nzunda anayekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.

  Bw. Tixon Tuliangine Nzunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Symthies Emmanuel Pangisa ambaye amestaafu.

  Baada ya kuapishwa, Mhe. Balozi Ramadhani Kitwana Dau na Makatibu Tawala wote watatu wamekula Kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda na kushuhudiwa na Rais Magufuli.

  Matukio yote yamefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es Salaam
  14 Septemba, 2016

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Rais Magufuli amwapisha Dkt. Ramadhan Dau kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia na Makatibu Tawala wa Mikoa watatu Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top