728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, September 2, 2016

  RAIS JPM ALIVYOMWAPISHA DOTO JAMES KUWA KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, mke wa Bw. Doto James, Bi. Irene Kahwili, Waziri Mkuu Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, mara baada ya tukio la kuapishwa kwa Katibu Mkuu huyo, Ikulu Jijini Dar es slaam, Septemba Mosi,
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, akipeana mkono na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, wakati wa tukio la kuapishwa kwake Ikulu, Jijini Dar es salaam, Septemba mosi 2016
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es salaam, Septemba mosi 2016

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es salaam, aliyekaa kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akishuhudia tukio hilo.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, akitia saini kiapo cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, mara baada ya kuapa, Ikulu, Jijini Dar es salaam, Septemba mosi, 2016  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, mara baada ya tukio la kuapishwa kwa Katibu Mkuu huyo, Ikulu Jijini Dar es slaam, Septemba Mosi, 2016


  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika, akimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, mara baada ya kuapishwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu, Jijini Dar es salaam, Septemba mosi, 2016
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akila kiapo cha uadilifu mbele ya Kamishna wa Maadili Jaji (Mst) Salome Kaganda, mara baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es salaam, Septemba mosi, 2016.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akila kiapo cha uadilifu mbele ya Kamishna wa Maadili Jaji (Mst) Salome Kaganda, mara baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es salaam, Septemba mosi, 2016.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akipeana mkono na Kamishna wa Maadili Jaji (Mst) Salome Kaganda, mara baada ya kula kiapo cha uadilifu baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es salaam, Septemba mosi, 2016.
  Katibu wa Chama cha wafanyakazi TUGHE, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenjeri James, akimkabidhi Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam, baada ya kuapishwa Ikulu ya Magogoni, kushika wadhifa huo.(Picha Zote na Wizara ya Fedha na Mipango).  Benny Mwaipaja, MoFP

  Dar es salaam

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amemwapisha Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, Ikulu, Jijini Dar es salaam, baada ya kumteua kushika wadhifa huo jana.

  Baada ya kuapishwa, Katibu Mkuu huyo amekula kiapo kingine cha maadili mbele ya Kamishna wa Maadili, Jaji (Mst.) Salome Kaganda, ambaye amemtaka kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu mkubwa ili kuisaidia nchi kufikia malengo yake ya kuwatumia wananchi katika sekta ya fedha na uchumi

  Bw. Doto James anachukua nafasi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Servacius Likwelile, ambaye Mhe. Rais Dkt. Magufuli, amesema atampangia kazi nyingine.

  Doto James, ambaye kitaaluma ni mchumi, alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango akishughulikia sera, atawaongoza manaibu makatibu wakuu wengine watatu walioko katika Wizara ya Fedha na mipango.

  Tukio hilo limehudhuriwa pia na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Peter Ilomo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika, na wakuu wa Mamlaka na Taasisi mbalimbali za serikali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: RAIS JPM ALIVYOMWAPISHA DOTO JAMES KUWA KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top