728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, September 17, 2016

  RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA TETEMEKO LA ARDHI LILILOTOKEA MKOANI KAGERA KUTOKA KWA WAZIRI MKUU.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea msaada wa fedha kiasi cha  dola laki mbili (USD 200,000) kutoka kwa Balozi wa Uganda hapa nchini Doroth Samali Hyuha wapili kutoka (kushoto) akiwa pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uganda Elibariki Maleko. Msaada huo umetolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa Tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
  bub2
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam.
  bub3
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akifatilia kwa makini taarifa iliyokuwa ikitolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhusu Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
  bub4
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kusoma taarifa kuhusu Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
  bub5
  Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  mchango wa fedha kiasi cha dola za Kimarekani laki mbili (USD 200,000) uliotolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni Ikulu jijini Dar es Salaam.
  bub6
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  bub7
  Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Uganda hapa nchini Doroth Samali Hyuha mara baada ya kuwasilisha mchango wa kiasi cha fedha Dola za Kimarekani laki mbili (USD 200,000) kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
  bub8
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Naibu Balozi wa Kenya hapa nchini Boniface Muhia mara baada ya kupokea salamu za pole kutoka kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na kwa misaada mbalimbali ambayo inatarajiwa kuwasili mkoani Kagera kutoka Kenya muda wowote. PICHA NA IKULU
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA TETEMEKO LA ARDHI LILILOTOKEA MKOANI KAGERA KUTOKA KWA WAZIRI MKUU. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top