728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, September 2, 2016

  RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI NA MKEWE JANETH WAZULU KABURI LA DK.OMAR ALI JUMA  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyewahi kuwa 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marehemu Dkt. Omar Ali Juma.Wawi Mchekeni, Chake Chake ,Pemba
  Mke wa Rais,Mama Janeth Magufuli akiomba dua kwenye kaburi la aliyewahi kuwa 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marehemu Dkt. Omar Ali Juma. lililopo Wawi Mchekeni, Chake Chake ,Pemba
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa ameambatana na Mkewe,Janeth Magufuli (hawaonekani pichani) wakisubiri kuweka mashada  ya maua na kuomba dua kwenye kaburi la aliyewahi kuwa 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marehemu Dkt. Omar Ali Juma. lililopo Wawi Mchekeni, Chake Chake ,Pemba.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Asubuhi ya leo tarehe 02 Septemba, 2016 amewasili Kisiwani Pemba ambapo majira ya Alasiri anatarajiwa kuzungumza na wananchi wa Pemba katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika katika uwanja wa Gombani ya Kale kisiwani hapa.

  Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Pemba kwa Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli ameelekea katika kijiji cha Wawi Bigilini kilichopo katika Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba ambako amezulu Kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marehemu Dkt. Omar Ali Juma.

  Dkt. Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wameweka mashada ya maua katika Kaburi la Marehemu Dkt. Omar Ali Juma na wameshiriki Dua ya kumuombea Marehemu iliyoongozwa na Viongozi wa Madhehebu ya Dini ya Kiislamu na Kikristo.

  Akizungumza mara baada Dua, Rais Magufuli amesema anamkumbuka Marehemu Dkt. Omar Ali Juma kwa ukarimu wake, upendo, kutojikweza, kutobagua watu na kudumisha amani katika siku zote za maisha yake.Dkt. Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kudumisha kwa vitendo amani aliyoisimamia Marehemu Dkt. Omar Ali Juma.

  "Mimi najua huko aliko Marehemu Dkt. Omar Ali Juma anaendelea kuliombea Taifa hili ili hiyo amani aliyoihubiri katika maisha yake, ili huo upendo aliousimamia katika maisha yake, ili huo uchapa kazi kwa ajili ya manufaa ya watanzania wote tuweze kuendeleza kwa mioyo yetu yote" Amesema Rais Magufuli.

  Aidha, Rais Magufuli amewashukuru Wanafamili wa Marehemu Dkt. Omar Ali Juma kwa uvumilivu na ustahimilivu wao tangu walipoondokewa na mpendwa wao.

  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Pemba
  02 Septemba, 2016

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI NA MKEWE JANETH WAZULU KABURI LA DK.OMAR ALI JUMA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top