728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, September 22, 2016

  Naibu Waziri Mhe.Anastazia afungua Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa TBC

    Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (aliyevaa Kitenge cha Kijani) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha RAAWU wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Shirika uliyofanyika Septemba 22,2016 Jijini Dar es Salaam.Aliyevaa Suti ya Bluu ni Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Utangazaji la Taifa Dkt.Ayoub Ryoba. Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (aliyevaa Kitenge cha rangi ya Kijani ) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe na wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha RAAWU wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika hilo uliyofanyika Jijini Dar es Salaam Septemba 22,2016.Aliyevaa Suti ya Bluu ni Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Utangazaji la Taifa Dkt.Ayoub Rioba. 
  Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha RAAWU wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) (hawapo pichani) katika ufunguzi wa mkutano wa Baraza hilo Septemba 22,2016 Jijini Dar es Salaam,katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa Dkt.Ayoub Ryoba. Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha RAAWU wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika hilo Septemba 22,2016 Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na na wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha RAAWU wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) (hawapo pichani)katika ufunguzi wa mkutano wa Baraza hilo Septemba 22,2016 Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa Kanda ya Kusini Bw.Asheri Chilewa akimwomba Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (hayupo pichani) kupitia Wizara yake kuandaliwe mkakati wa kufundisha lugha ya Kiswahili fasaha kwani kumekuwa na makosa mengi yanayojitokeza katika matumizi ya Kiswahili, katika mkutano na wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha RAAWU wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) uliyofanyika Septemba 22,2016 Jijini Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali ya wafanyakazi. Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC)Dkt. .Ayoub Ryoba akizungumza namna walivyoweka mikakati ya kutatua changamoto za wafanyakazi wa Shirika hilo kwa Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) katika mkutano na wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha RAAWU wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) uliyofanyika Septemba 22,2016 Jijini Dar es Salaam. 
  Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi RAAWU Taifa Bw.Felician Maige akimuomba Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa kwanza kulia) kuzungumza na Uongozi wa Shirka la Utangazaji la Taifa kwa kuwapatia ajira za kudumu wafanyakazi waliyokuwa hawana mikataba kwa muda mrefu,katika Mkutano na wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha RAAWU wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) uliyofanyika Jijini Dar es Salaam Septemba 22,2016.

  ………………………………………………………….
  Na Anitha Jonas – WHUSM- Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo amewaahidi Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kufuatilia malimbikizo ya mishahara yao na kuhakikisha wanalipwa. 

  Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC ) uliyolenga kujadili bajeti ya mwaka 2016/2017 iliyopitishwa na Bunge na kuweka mikakati ya namna Shirika litakavyoweza kupata pesa nakuweza kujiendesha pamoja na namna ya kuboresha huduma ya matangazo.
  “Natambua TBC ina wafanyakazi zaidi ya mia sita (600) nawasihi mtakapotoka hapa mkawarejeshee wenzenu mliyojifunza na mkawaeleze mipango mliyoamua kwa niaba yao,”alisema Mhe.Anastazia. 

  Akiendelea kuzungumza katika Mkutano huo Mhe.Anastazia aliupongeza uongozi wa TBC kwa kuandaa Harambee ya kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera kwani wameonyesha uzalendo wao wa kuona changamoto zilizopo katika kurekebisha miundombinu iliyoharibika pamoja na kuwasaidia wakazi walioathirika mahitaji muhimu.
  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt.Ayoub Ryoba alisema shirika lina malengo ya kuwafikia Watanzania wote na kuhakikisha linawaunganisha kwa Taarifa mbalimbali,pamoja na kuandaa vipindi vyenye maudhui yanayogusa watu wote.

  Pamoja naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi RAAWU Taifa Bw.Felician Maige alimuomba Mhe.Naibu Waziri kuzungumza na uongozi wa Shirika hilo kuhusu kuwapatia ajira za kudumu au mikatabu baadhi ya wafanyakazi waliyofanya kwa muda mrefu kama vibarua. 

  Kwa upande wa mmoja wa Wafanyakazi wa TBC Bw. Asheri Chilewa alimuomba Naibu waziri huyo kupitia Wizara yake na Taasisi yake ya Kiswahili kuundwe mkakati utakaosaidia kufundisha jamii lugha ya Kiswahili kwa ufasaha kwani kwa hivi karibuni kumekuwa na upotoshwaji wa matumizi ya lugha hiyo kwa kiasi kikubwa na maneno kutumika isivyo sawa .
  Huku akitoa mfano wa namna watu wanasema mtu amepoteza maisha pale anapofariki ambapo siyo sahihi kwani maisha ya mtu hayapotei.
  Hata hivyo Naibu Waziri aliueleza Uongozi wa TBC kuwa Serikali inaelewa changamoto wanazopitia na kwa sasa inashughulikia suala hilo kwa kuona ni namna gani kupitia mapato ya Kampuni ya Startimes yatakavyoweza kuchangia uendeshaji wa shirika hilo na mpaka mwakani mkakati huo utakuwa umekamilika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Naibu Waziri Mhe.Anastazia afungua Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa TBC Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top