728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, September 20, 2016

  MKUU WA MKOA WA ARUSHA AMPA WIKI MBILI MKURUGENZI WA JIJI KUHAKIKISHA WALIMU WOTE WANAODAI SEREKALI WALIOPO NDANI YA JIJI LA ARUSHA WANALIPWA FEDHA ZAO


  MKUU wa mkoa Arusha Mrisho Gambo akiongea na walimu wote wa shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha ,waratibu elimu,wakaguzi elimu pamoja na maafisa elimu kata .
  Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro akiwa anaongea na walimu waliohuthuria mkutano huo.

  Habari picha na Woinde Shizza,Arusha

  MKUU wa mkoa Arusha Mrisho Gambo amemuagiza mkurugenzi wa jiji la
  Arusha, Athumani Kihamia kulipa madeni yote wanayodai walimu ya
  milioni 154 ndani ya wiki mbili ambayo wamekuwa wakidai serikali
  kuu kwa muda mrefu bila kulipwa na hivyo kusababisha walimu hao
  kukata tamaa ya ufundishaji wanafunzi .

  Gambo alitioa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na walimu wote wa
  shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha ,waratibu elimu,wakaguzi elimu pamoja na maafisa elimu kata katika mkutano wa kujua changamoto zinazowakabili walimu hao ili zipatiwe ufumbuzi.

  Alisema kuwa walimu wamekuwa wakifundisha katika mazingira magumu na kwamba hadi sasa wapo walimu wa shule za msingi wanaoadai madeni ya likizo na mengineyo yenye gharama ya milioni 154 ambapo serikali kuu
  ndio inayopaswa izilipe na hadi sasa hawajalipwa jambo ambalo
  linawafanya walimu hao kupoteza muda wa kufundisha na kufuatilia kila
  siku madeni hayo.

  “mkurugenzi nakupa muda wa wiki mbili deni hili la milioni 154 kwa
  ajili ya walimu akikisha zinalipwa haraka iwezekanavyo wakishalipwa
  ndio upambane na serikali kuu ufidie hapo zilikotolewa kwani
  haiwezekani walimu wapoteze muda kila siku wakifuatilia tu madeni huku
  wakiwa wameacha vipindi bila kufundisha wanafunzi wetu”alisema Gambo.

  Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji hilo,Athumani Kihamia akijibu agizo
  hilo alilopewa na mkuu wa mkoa alisema kuwa fedha hizo ambazo ni
  madeni hayo zinapaswa zitokee serikali kuu na kwamba atahakikisha
  kuwa ndani ya muda wa wiki mbili atazilipa kupitia fedha za ndani za
  halamshauri hiyo ili zikija zirejeshwe.

  Alifafanua kuwa deni hilo atalipa kutoka kwenye fedha alizoziokoa
  ambazo zilikuwa zinalipwa kinyume cha sheria kwa madiwani ambapo
  kiasi cha milioni 130 zilizokuwa zinatumika kuwalipia madiwani
  mafuta ,simu pamoja na nauli zitaelekezwa kulipa walimu hao madai
  yao ili waweze kujikimu na hali wanayokabiliana nayo.

  ‘‘Fedha ambazo zimeokolewa kwa ajili ya mafuta ni milioni 40.8,fedha
  za simu za madiwani milioni 61.2,nauli iliyookolewa milioni 28 ambapo
  jumla ni milioni 130 ambazo zimelipwa kinyume hivyo fedha hizi
  zinaelekezwa kwa walimu wa msingi na sekondari ikiwa ni madeni
  wanayodai halmashuri hii ambapo fedha zinasubiriwa serikali kuu lkni
  tumeona tuwatangulizie hizi fedha ili wajikimu na waweze kufundisha
  watoto wetu vizuri”alisema Kihamia .

  Kihamia alisema kuwa watatanguliza fedha hizo kwa walimu hao wakati
  wakiwa wanasubiria fedha toka serikali kuu ili waendelee kujikimu
  kwani zimeokolewa katika mianya ambayo zilikuwa zinateketea hivyo
  zitaongeza ufanisi kwa walimu katika kufundisha wanafunzi na akili
  zao na kufanya akili zao kuzielekeza kwa wanafunzi ili wapate elimu
  bora.

  Baadhi ya walimu hao wakieleza kero zao walisema kuwa wanakabiliwa na
  tatizo la kutopandishwa madaraja kwa waliokaa kazini muda mrefu huku
  wengine walioingia kazini muda mfupi wakiwa wanapandishwa madaraja
  bila kujua vigezo hivvyo kumwomba mkuu wa mkoa kuingilia swala hilo.  wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa jiji la ArushaAthumani Kihamia akiwa anasikiliza kwa makini malalamiko ya walimu hao


  picha ya juu na chini ni walimu waliouthuria mkutano huo wa mkuu wa mkoa uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa AICC uliopo mkoani Arusha


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MKUU WA MKOA WA ARUSHA AMPA WIKI MBILI MKURUGENZI WA JIJI KUHAKIKISHA WALIMU WOTE WANAODAI SEREKALI WALIOPO NDANI YA JIJI LA ARUSHA WANALIPWA FEDHA ZAO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top