728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, September 18, 2016

  MCHEZAJI BORA WA MWEZI AUGUST WA SIMBA SPORT CLUB AKABIDHIWA TUZO YAKE
  Mchezaji bora wa Klabu ya Simba kwa mwezi Agosti, 2016 Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' amekabidhiwa tuzo yake mbele ya mashahiki waliokujakushuhudia mchezo wa kati ya Azam Fc na Simba Sc. Pamoja na tuzo hiyo Zimbwe Jr pia amekabidhiwa Tsh 500,000/= kama sehemu ya zawadi kwa mchezaji bora. Hii ni tuzo ya kwanza kutolewa kwa msimu huu 2016/2017 ambapo ilikabidhiwa kwa Zimbwe Jr na Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG Group Imani Kajula pamoja na Makamu wa Rais wa Simba Geophrey Nyange kabla ya mchezo wa kuanza, mchezo ambao ulikwisha kwa Simba kuibuka kidedea kwa kuifunga Azam FC kwa goli moja bila, goli lililofungwa na Shiza Kichuya Dakika ya 68 Kipindi cha Pili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MCHEZAJI BORA WA MWEZI AUGUST WA SIMBA SPORT CLUB AKABIDHIWA TUZO YAKE Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top