728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, September 2, 2016

  MBWA DOMO BAYA MLINZI NAMBA ONE WA RAS MAKUNJA ANATAFUTWA KAPOTEA


  MBWA Sajent Domo Baya mlinzi namba moja wa Ras Makunja anatafutwa!
  Katika makao ya mkuu wa Ngoma Africa band kamanda Ras Makunja hali imekuwa si shwari baada ya mbwa aina ya Bulld dog mwenye jina la sajent Domo Baya mlinzi namba moja wa Ras Makunja ametoroka lindoni kwa muda wa siku tatu sasa na kikosi cha kuangalia wanyama cha mji wa Oldenburg kinamtafuta mbwa huyo mwenye umri wa miaka 14 ambaye mara nyingi ni mwenye vituko pale anapochoka kulinda.

  mmiliki wa mbwa huyo kamanda Ras Makunja alikaliliwa akimlalamikia mlinzi wake huyo kwa kudai kuwa “kama kachoka kazi atamfuta” mwanamuziki huyo anamlalamikia mlinzi wake huyo kuwa kuwa siku hizi ana tabia za uzembe sana “Kishanigombanisha na jirani baada ya kuvamia

  swimming pool ya jirani” Kamanda Ras Makunja wa Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni analalamika.lakini sikiliza kazi zao at www.ngoma-africa.com
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  1 comments:

  1. Amuachishe kazi amlipe mafao yake arudi kwao kwani kashaonekana ni mzembe WA kazi

   ReplyDelete

  Item Reviewed: MBWA DOMO BAYA MLINZI NAMBA ONE WA RAS MAKUNJA ANATAFUTWA KAPOTEA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top