728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, September 26, 2016

  MASAUNI AZINDUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI, KITAIFA MJINI GEITA LEO


  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akitoa hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani alioizindua Kitaifa mjini Geita leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Hatutaki Ajali, Tunataka Kuishi”. Katika hotuba yake, Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  mass2
  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimsikiliza Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka Makao Makuu, Koplo Faustina Ndunguru wakati alipokuwa anatoa maelezo jinsi magari mbalimbali yanavyovunja sheria za barabarani. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa maonyesho hayo yanayofanyika Kitaifa mjini Geita, Mhandisi Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  mass3
  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiyaangalia maandamano ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo yanafanyika Kitaifa katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita, yalipokuwa yanaingia katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuadhimisha wiki hiyo. Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  mass4
  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimpa zawadi ya Kombe la Ushindi wa kwanza Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam, Veronica Innocent, ambaye alishinda nafasi ya kwanza katika uchorani wa picha zinazoonyesha usalama barabarani ambayo zilipambanishwa katika shule za Mkoa wa Dar es Salaam na Geita. Masauni aliyazindua Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, ambayo yanafanyika Kitaifa, katika Viwanja vya CCM Kalangalala, mjini Geita. Masauni katika hotuba yake aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  mass5
  Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga akizungumza katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inayofanyika Kitaifa katika Viwabya vya CCM Kalangalala mjini Geita. Maadhimisho hayo yalizinduliwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia).
  mass6
  Washiriki wa maonesho (waendesha bodaboda) wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyozinduliwa katika Viwanja vya CCM Kalangalala, mjini Geita leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Hatutaki ajali tunataka kuishi salama”. Maadhimishjo hayo yalinduliwa na Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni. Katika hotuba yake Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe.
  mass7
  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi cheti cha ushiriki, Mwakilishi wa Kampuni ya Bia nchini (TBL), Amanda Walter.  toa hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani alioizindua Kitaifa mjini Geita leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Hatutaki Ajali, Tunataka Kuishi”. Katika hotuba yake, Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MASAUNI AZINDUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI, KITAIFA MJINI GEITA LEO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top