728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, September 3, 2016

  MAMLAKA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII (SSRA) ILIPOSHIRIKI MAONESHO YA WIKI YA FEDHA JIJINI DAR ES SALAAM


  Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde Msika (katikati) na Bw. Kenneth Batanyita (kushoto), wakitoa maelezo kuhusu Hifadhi ya Jamii kwa mgeni aliyetembelea banda la SSRA, wakati wa maonesho ya Wiki ya Fedha, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
  Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde Msika akitoa maelezo na kugawa vijarida kuhusu hifadhi ya Jamii kwa baadhi ya wageni waliotembelea banda la SSRA katika maonesho ya Wiki ya Fedha, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Afisa wa SSRA, Bi. Amina Ally akitoa mada katika Semina ya uhamasishaji wa Hifadhi ya Jamii kwa wajasiriamali wadogo walioshiriki katika mafunzo yaliyokuwa yakitolewa katika Wiki ya Fedha yaliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja hivi karibuni.
  Maofisa wa Mamlaka, Bi. Imani Masebu (kushoto) na Bi. Agnes Lubuva (kulia) wakitoa maelezo kuhusu umuhimu wa Hifadhi ya Jamii kwa wajasiriamali wadogo waliotembelea banda la SSRA katika maonesho ya wiki ya Fedha hivi karibuni.
  Afisa wa Mamlaka Bw. Athumani Juma akigawa vipeperushi na vijarida vya uhamasishaji wa umuhimu wa kujiunga na Hifadhi ya Jamii kwa wajasiriamali wadogo waliotembelea banda la SSRA katika maonesho hayo, hivi karibuni.
  Afisa wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Ally Masaninga akitoa maelezo kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka pamoja na kugawa vipeperushi kwa washiriki waliotembelea Banda la SSRA katika maonesho ya wiki ya Fedha, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

  Afisa wa SSRA, Bw. Frank Kilimba akitoa maelekezo kuhusu Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa wageni waliotembelea banda la Mamlaka hiyo, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini.
  Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (wa pili kushoto), katika meza kuu akiwa na viongozi wa maonesho ya wiki ya Fedha pamoja na wawakilishi wa Mashirika na Taasisi mbalimbali ikiwemo SSRA, wakifuatilia kwa makini risala toka kwa wajasiriamali (hawapo pichani), katika siku ya kilele cha maonesho ya Fedha, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MAMLAKA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII (SSRA) ILIPOSHIRIKI MAONESHO YA WIKI YA FEDHA JIJINI DAR ES SALAAM Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top