728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, September 9, 2016

  MAJIBU YA SERIKALI KATIKA MASWALI MBALIMBALI YA WABUNGE LEO


  #Serikali imesema katika bajeti ya mwaka 2015/2016, imetumia shilingi milioni 144 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya mradi wa maji kutoka chanzo cha mto Maswila ili kukidhi mahitaji ya maji kwa wakazi wa Tukuyu.

  #Serikali imesema miradi mingi ya maji inatekelezeka kwa kuwa imejipanga katika makusanyo ya mapato ambayo yatasaidia kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa maendeleo ya wananchi.

  #Serikali imesaini Mkataba kwa ajili ya kusambaza mtandao wa mabomba ya maji Dar es Salaam ambapo kazi imeanza maeneo ya Kiluvya na kuendelea  maeneo mengine ikiwemo mji mkongwe wa Bagamoyo.

  #Serikali inatambua changamoto za kiteknolojia, hususani ununuzi kupitia mtandao, hivyo imechukua hatua ya kuwaongezea wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato uwezo wa kukusanya kodi kwenye biashara zinazofanyika kwa njia ya mtandao.

  #Serikali imetoa fursa kwa vikundi vya VICOBA kusajiliwa na BRELA pamoja na Halmashauri za Wilaya na imekamilisha mapitio ya marekebisho ya Sera ya Huduma Ndogondogo za Kifedha na Sheria yake (Tanzania Bara) na Sera ya Huduma Ndogondogo za Kifedha (Zanzibar) zinazotarajiwa kuweka mwongozo rasmi wa usajili wa VICOBA na uendeshaji wake.

  #Serikali imeanza kutekeleza ujenzi wa njia ya umeme itakayounganisha Wilaya ya Liwale na Wilaya ya Nachingwea ambazo kwa sasa zinatumia umeme kutoka kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia kilichopo Mtwara.

  #Serikali imeanza kutatua changamoto ya umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara kwa kuunganisha mikoa hiyo kwenye gridi ya Taifa na kuweka njia mpya ya msongo mkubwa wa KV. 400 hatua ambayo itaondoa changamoto hiyo na haitachukua muda mrefu.

  Imeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MAJIBU YA SERIKALI KATIKA MASWALI MBALIMBALI YA WABUNGE LEO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top