728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, September 23, 2016

  LOWASSA AISIFU SERIKALI URATIBU MAAFA KAGERA


  Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa akisalimiana na
  Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Generali Salum Kijuu alipomtembela leo ofisini kwake kumpa pole kutokana na athari ya tetemeko la ardhi katika mkoa wake


  Na Mwandishi Wetu-KAGERA.

  Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa ameipongeza Serikali kwa namna ilivyojipanga kukabiliana na athari za tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo.


  Bw. Lowassa amesema hayo kupitia salamu zake alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Generali Salum Kijuu, ofisini kwake kumpa pole kutokana na athari zilizotokana na tetemeko hilo.


  “Napenda nikupongenze mkuu wa mkoa kwa namna ulivyokabili tukio hili, wala hatukuwa na mashaka wewe ni mtaalam wa majeshi wa siku nyingi kwa hiyo jambo hili limempata mwenyewe mpiganaji na tunaona kwa pamoja mmelishikilia vizuri,” alisema Lowassa.


  Adha Mhe. Lowassa alisema kuwa suala hili ni kubwa na halipaswi kuiachia Serikali peke yake katika kulikabili nalo kwani madhara yanaonekana ni makubwa hivyo watanzania wote wana budi kuwasaidia waathirika.


  Katika kushirikiana na wananchi wa Kagera, Bw. Lowassa ameahidi kutoa mifuko 400 ya saruji kwa ajili ya ujenzi ya miundombinu iliyoharibika.


  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja, Generali Salum Kijuu ameendelea kuwasisitiza watanzania kuchangia kile walichonacho ili kusaidiana na serikali katika kuwafariji waathirika wa tetemeko hilo.


  “Tunashukuru watanzania kwa misaada wanayoendelea kutoa kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko ila bado tunaendelea kuwasisitiza tuendele kujitoa kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye mahitaji,” alisema  Meja Generali Salum Kijuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: LOWASSA AISIFU SERIKALI URATIBU MAAFA KAGERA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top