728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, September 18, 2016

  KUFUATIA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA WAZIRI MWIGULU AAMURU WAFUGWA WAHIMISHWE GEREZA


    Waziri Mwigulu Nchema akipata maeleozo mafupi kuhusiana na ofisi ya Askari wa doria majini (Marine police) iliyobomoka kutokana na tetemeko la ardhi
   Waziri Mwigulu Nchema akikagua ofisi ya Askari wa doria majini(Marine police) iliyobomoka kutokana na tetemeko la ardhi
  Waziri Mwigulu Nchemba akikagua makazi ya askari magereza wa Kitengule zilizobomoka kutokana na tetemeko la ardhi. 
   Waziri Mwigulu Nchemba akiangali sehemu ya nyuma ya gereza la Kitengule ambalo ukuta wake umebomoka kutokana na tetemeko la ardhi.


  Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera.

  WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba amemtaka mkuu wa magereza mkoa wa Kagera(RPO) kamishna mwandamizi Jeremiah Nkonda kuwahamisha wafungwa walioko katika gereza la Kitengule la wilayani Karagwe na kuwapeleka gereza jirani la Mwisa,Kutokana na tetemeko la ardhi lililo tokea hivi karibuni mkoani hapa na kuharibu miundombinu na mabweni ya kulala wafungwa katika gereza hilo.

  Waziri Nchemba alisema kauli hiyo baada ya kufanya ziara ya siku moja  Mkoani hapa na kutembelea taasisi zilizo chini ya wizara yake Kwa lengo la kuona uharibifu uliojitokeza kutoka na tetemeko hilo .

  "Nimetembelea magereza yetu lakini gereza la Kitengule limeharibika sana, kuta zimeanguka mabweni yameharibika  Kwa kiwango kikubwa kiasi kwamba hawapaswi kuishi watu kwahiyo,naagiza mkuu wa magereza hapa kuwahamishia wafungwa hawa katika gereza la Mwisa lenye mabweni manne yaliyoko  wazi"Alisema Nchemba.

  Alisema ndani ya wiki moja zoezi hilo liwe limekamilika kwani wakiendelea kuwaaacha wafungwa hao humo ni hatari kwani wanaweza kudondokewa na kuta zinazoning'inia na kusababisha kuwapoteza watu hao.

  Alisema kutokana na tukio hilo Wizara inaandaa mpango wa Muda mrefu wa kujenga bweni kubwa litakalokuwa na uwezo wa kubeba wafungwa 400 Kwa wakati mmoja kwani hilo ni gereza  la kikazi ambalo linabeba watu wengi.

  Mkuu wa magereza mkoa wa Kagera kamishna mwandamizi Jeremiah Nkonda alisema kilichochangia Sana kushuka Kwa kuta hizo ni kwamba matofali yaliyojenga kuta hizo yanaonekana yalijengwa Kwa tofali mbichi kwahiyo Kwa halii hiyo haitowezekana kufanya ukarabati bali nikuhakikisha Wamebomoa mabweni hayo na kujenga upya.

  Alisema gereza hilo lilikuwa na uwezo wa kubeba wafungwa 380  Kati ya hao 100 wako Kwenye kambi ndogo ambapo 280 ndo watakaohamishiwa katika gereza la Mwisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: KUFUATIA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA WAZIRI MWIGULU AAMURU WAFUGWA WAHIMISHWE GEREZA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top