728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, September 16, 2016

  Kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini watatu na dereva teksi mmoja: Christopher Bageni ahukumiwa kunyongwa hadi kufa, zombe na wenzie wawili waachiwa huru

   Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Ilala Christopher Bageni amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya Mahakama ya Rufani Tanzania kutengua hukumu iliyomwachia huru na kumtia hatiani kwa kosa la mauaji ya wafanyabiashara wa madini watatu na dereva teksi mmoja.
  Kadhalika mahakama hiyo imewaachia huru  Mkuu wa Upelelezi wa zamani (wakati huo Mkoa wa Dar es Salaam) (RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi  mstaafu Abdallah Zombe na wenzake wawili baada ya ushahidi wa rufaa hiyo kushindwa kuwatia hatiani.

  Mara baada ya hukumu kusomwa, ghafla Bageni aliduwaa wakati wenzake wakimkumbatia huku  wakibubujikwa na machozi wakiwa kizimbani. 
  Wanaodaiwa kuwa wanafamilia wa washtakiwa hao waliangua vilio huku washtakiwa wenzake walisikika wakieleza masikitiko yao. Wengine walisikika wakisema angejua asingekuja mahakamani kusikiliza hukumu hiyo.
  “Namshukuru Mungu...Lakini nasikitika kwa Bageni kukutwa na hatia sina raha kabisa....” alisema ASP Makele wakati akitoka katika ukumbi namba moja wa mahakama hiyo. 

  Akizungumza baada ya hukumu hiyo,  ACP mstaafu Zombe alisema anamshukuru Mungu na kuhusu Bageni alisema hana cha kuzungumzia.
  Hukumu hiyo imesomwa leo na Msajili wa mahakama hiyo Mhe. John Kahyoza baada ya rufani iliyokatwa na upande wa Jamhuri  kusikilizwa na jopo  la majaji watatu likiongozwa na Mwenyekiti, Jaji Bernard Luanda, Jaji Sauda Mjasiri na Jaji Semistocles Kaijage.

  Msajili alisema awali Mahakama Kuu iliyoketi chini ya Jaji Salum Massati (wakati huo kabla ya kupanda kuwa jaji wa rufani), ilimuona Zombe na wenzake hawana hatia na kwamba haiwezi kuwahukumu kwa kosa la kusaidia kufanyika mauaji hayo.
  Alisema Mahakama ya Rufani inakubaliana na Jaji Massati  kwamba mtuhumiwa hawezi kutiwa hatiani bila kuthibitisha mtu aliyetenda kosa hajashtakiwa na kutiwa hatiani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini watatu na dereva teksi mmoja: Christopher Bageni ahukumiwa kunyongwa hadi kufa, zombe na wenzie wawili waachiwa huru Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top