728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, September 21, 2016

  KAMPUNI YA SKOL CONTRACTORS BUILDING LIMITED YASAIDIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA.

   Mwenyekiti wa Kampuni ya Skol Building  Contractors Limited Bw.Vincent Massawe (kushoto) akikabidhi Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye(kulia) kiasi cha Shilingi Milioni Kumi taslimu leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia wakazi wa Mkoa wa Kagera waliyoathirika na tetemeko la ardhi liliotokea hivi karibuni.
   Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kulia) akifurahia jambo mara baada ya kupokea msaada wa Shilingi Milioni Kumi uliyotolewa na Kampuni ya SKOL Bulding Contractors Limited  Ofini kwake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya  kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera hivi Karibuni (Kushoto) ni Bw.Vincent  Massawe kutoka Kampuni hiyo mara baada ya kukabidhi pesa hizo. 

  Na Shamimu Nyaki – WHUSM
  WAZIRI wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amepokea  kiasi cha Shilingi Milioni Kumi kutoka  Kampuni ya Skol Building  Contractors Limited. 

  Akipokea fedha hizo leo Jijini Dar es Salaam kutoka kwa Mwenyekiti  wa Kampuni hiyo Bw. Vincent Peter Masawe  Waziri  Nnauye amemthibitishia kuwa pesa hizo zitawasilishwa  kwa waathirika wa tetemeko hilo ili zitatue changamoto zinazowakabili.

  “Ninashukuru sana kwa msaada wenu mmetambua changamoto wanazopata wenzetu,niwaombe Watanzania wote tuendelee kujitoa kuwasaidia ndugu zetu waliopata maafa haya”.Alisema Mhe.Nnauye.

  Aidha Mwenyekiti wa kampuni hiyo Bw.Vincent Peter Masawe amesema Kampuni yao imeguswa na matatizo waliyopata wakazi  hao wa Kagera na ndio maana  wameamua kuwasaidia ili hali zao za maisha zireje kama zamani.

  “Tumeamua kuwasaidia wenzetu na tunaomba wafanyabiashara na Watanzania kwa ujumla popote walipo waguswe na jambo hili na waunge mkono Serikali katika juhudi zake za kuwasaidia waathirika wa tetemeko hili”. Aliongeza Bw.Masawe.

  Katika hatua nyingine Mhe. Waziri amewakaribisha wananchi wote katika harambee ya kuchangia waathirika hao iliyoandaliwa na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) itakayofanyika Septemba 21 mwaka huu jioni katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo Jijini Dar es Salaam
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: KAMPUNI YA SKOL CONTRACTORS BUILDING LIMITED YASAIDIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA. Rating: 5 Reviewed By: MICHUZI BLOG
  Scroll to Top