728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, September 26, 2016

  Jumla ya Tsh 187 Million zapatikana mchezo wa kirafiki baina ya Wabunge mashabiki wa Yanga na Simba leo uwanja wa Taifa jijini Dar

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kukabidhi kikombe kwa washindi katika mchezo wa kirafiki baina ya Wabunge mashabiki wa Yanga na Simba ambapo Yanga wameifunga simba 5- 2 

  Katika mchezo huo Jumla ya Tsh 187 Million zimepatikana ambazo zitakabidhiwa rasmi kwa waziri mkuu ili kuwasilishwa kwa waathiriwa na tetemeko la Ardhi lililotokea mjini Bukoba mkoani Kagera, na kupelekea kupoteza maisha ya wananchi 17 na kujeruhi wengine wengi na kuharibu nyumba na miundo mbinu mbalimbali.
  way2
  Mwenyekiti wa timu ya wabunge Mh. William Ngeleja akizungumza jambo mara baada ya mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.Katika mchezo huo wa kirafiki Wabunge washabiki wa Yanga waliibuka washindi kwa kuwafunga mashabiki wa simba goli 5-2
  way3
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akikabidhi kikombe kwa wabunge mashabiki wa timu ya Yanga kwenye uwanja wa taifa leo.
  way4
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde wakati akiwapongeza wabunge mashabiki wa Yanga kwa ushindi mnono wa magoli 5-2  dhidi ya Wabunge mashabiki wa Simba kwenye uwanja wa Taifa leo.
  way5
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akisalimiana na MWIGULU Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani, wakati akiwapongeza wabunge mashabiki wa Yanga kwa ushindi mnono wa magoli 5-2  dhidi ya Wabunge mashabiki wa Simba kwenye uwanja wa Taifa leo.
  way6
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akikabidhi kombe kwa wabunge mashabiki wa timu ya Yanga mara baada ya ushindi wao dhidi ya wabunge mashabiki wa timu ya Simba kwenye uwanja wa Taifa leo.
  way7
  Wabunge Mashabiki wa Yanga wakishangili na kombe lao mara baada ya kuibuka washindi wa mchezo huo leo kwenye uwanja wa Taifa.
  way8
  Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni ya leo.
  way11
  Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai akiwavisha nishani wabunge mashabiki wa Simba mara baada ya mchezo huo kumalizika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Jumla ya Tsh 187 Million zapatikana mchezo wa kirafiki baina ya Wabunge mashabiki wa Yanga na Simba leo uwanja wa Taifa jijini Dar Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top