728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, September 15, 2016

  Jokate awaomba Watanzania kuchangia wahanga wa tetemeko Kagera

  Mrembo, msanii wa filamu na mwanamuziki, Jokate Mwegelo ametoa wito kwa jamii, mashirika na watu binfasi kujitolea kusaidia wahanga wa tetemeko la Ardhi lililoikumba mkoa wa Kagera na kusababisha vifo na baadhi ya watu kukosa makazi ya kuishi.

  Jokate alitoa wito huo jana wakati wa kutangaza mikakati yake ya kusaidia wahanga wa tetemeko hilo kwa kushirikiana na Taasisi ya GSM Foundation. Alisema kuwa tikio hilo ni kubwa na lemeleta majonzi kwa baadhi ya familia na kuwaomba wadau kuungana kusaidia kuondoa changamoto zinazowakumba wahanga.

  Alisema kuwa wakati anajipanga chini ya msaada wa GSM Foundation, ameamua kutoa rai kwa watanzania ikiwa pamoja na wanamichezo, wasanii, wanamuziki na wadau wengine mbalimbali kuchangia ili kuondoa changamoto hizo.

  “Kwa kweli hali si nzuri kabisa, mimi kama msanii na ni Mtanzania, nimeguswa na kuamua kuingia mtaani kuhamasisha watu binafsi, makampuni na asasi mbalimbali kuunga mkono juhudi za serikali kusaidia wahanga wa tetemeko hilo,” alisema Jokate.

  Alisema kuwa ni jukumu la kila Mtanzania kuungana katika tatizo hilo ambalo pia limeharibu baadhi ya shule na kusababisha wanafunzi kukosa sehemu ya kupata elimu. “Kwa wasanii, warembo na wanamuziki, ni wakati muafaka sasa kusaidia na kufanya mrejesho wa mapato yetu kwa jamii kwa kusaidia wahanga,” alisema.

  Alifafanua kuwa suala hili si kwa watu wenye uwezo,tu, bali hata watu wenye kipato kidogo linawahusu kwani chochote walichonacho kama nguo, vyombo vya nyumbani, vitanda, magodoro, chakula, sabuni, mafuta na vitu vingine vinahitajika kwa wahanga wa tetemeko hilo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Jokate awaomba Watanzania kuchangia wahanga wa tetemeko Kagera Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top