728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, September 22, 2016

  Jaji amkabidhi Lukuvi ripoti ya Mgogoro wa Mabwegere


  Jonas Kamaleki- MAELEZO

  Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Jacob Mwambejele amemkabidhi Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi ripoti ya uchunguzi baada kukamilika kwa uchunguzi huo.

  Tukio hilo limefanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo ripoti iliyohusu uchunguzi wa Mgogoro wa muda mrefu kuhusu kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani, Kilosa, mkoani Morogoro.

  Katika makabidhiano hayo Jaji Mwambejele amesema kwa kushirikiana na timu yake, Wizara ya Ardhi, Vijiji vya wilayani Kilosa na uongozi wa Mkoa wa Morogoro wamekamilisha ripoti hiyo ndani ya siku 60 kama adidu za rejea zilivyowataka.

  Jaji Jacob Mwambejele amesema uchunguzi huo uliangalia baadhi ya mambo ikiwemo kama uanzishwaji wa kijiji cha Mabwegere ulianzishwa kisheria na sheria zilifuatwa katika uanzishwaji huo, kama ulikuwepo usahihi wa kisheria katika upimaji wa eneo hilo na kama wanavijiji walishirikishwa, alisema Lukuvi.

  Jaji huyo ameyataja maeneo mengine ya uchunguzi huu kuwa yalikuwa pamoja na kuchunguza kama upimaji ulizingatia mipaka, kuchunguza maeneo mengine yenye migogoro na kuchunguza jambo jingine lolote ambalo litasaidia katika kuleta suluhu ya mgogoro huo.

  Kwa upande wake, Waziri Lukuvi ametoa shukrani zake kwa Jaji Mwambejele na timu yake, waziri Lukuvi amesema ripoti hiyo imekalika kwa wakati na inataraji kumaliza mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 25.

  “Mapendekezo yaliyotolewa ndani ya ripoti ya Jaji, tutayafanyia kazi haraka iwezekanavyo ili kumaliza mgogoro wa Mabwegere ambao umedumu kwa miaka mingi,” alisema Lukuvi.

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi mapema mwaka huu alimteua kwa mamlaka yake chini ya kifungu 18 (1) cha Sheria ya Ardhi sura 113 Jaji Jacob Mwambejele wa Mahakama Kuu- Kitengo cha Biashara kuchunguza mgogoro wa Kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani vya Mfuru, Mbigiri, Mandengwa, Dumila , Matongolo na Maboiga vilivyopo Wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro ili kupata suluhisho la kudumu la mgogoro huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Jaji amkabidhi Lukuvi ripoti ya Mgogoro wa Mabwegere Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top