JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


DKT. MUSA MGWATU ATEULIWA KUWA MTENDAJI MKUU WA TEMESA.

Share This


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchuzi na Mawasiliano (Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame M. Mbarawa(Mb), amemteua Dkt. Musa Mgwatu kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA). 

Dkt. Mgwatu amechukua nafasi ya Mhandisi Marcellin Magesa  ambaye amepangiwa majukumu mengine  Wizarani.

Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Mgwatu alikuwa  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Hodhi la Rasilimali za Reli (RAHCO).

Katika hatua nyingine Profesa Mbarawa amemteua Bw. Masanja Kadogosa ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Kukaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa RAHCO.
Uteuzi huo unaanza mara moja.
Imetolewa na
Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad