728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, September 28, 2016

  DK. SHEIN AFANYA UTEUZI

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, leo amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali katika taasisi za serikali.

  Dk. Shein amemteua Dk. Ahmed Mohammed Khatib kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi ya Zanzibar.

  Aidha, Ndugu Hamad Bakari Mshindo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Habari wakati Dk. Wakil Idriss Abdulwakil, anakuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Mnazimmoja.

  Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyosainiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, uteuzi huo unaanza leo tarehe 28, Septemba, 2016.

  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO-ZANZIBAR

  28 Septemba, 2016

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: DK. SHEIN AFANYA UTEUZI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top