728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, September 14, 2016

  Bodi ya Filamu yaahidi ushirikiano uanzishwaji wa Mradi wa TYEEO Barazani Entertainment.

  Na: Frank Shija, MAELEZO

  SERIKALI imepongeza juhudi za wadau wa Tasnia ya Filamu nchini kutokana na jitihada zao katika kuhakikisha tasnia hiyo inakuwa na kuwaletea maendeleo endelevu ikiwemo Ajira za uhakika kwa vijana.

  Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mktendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF) Bibi. Joyce Fissoo alipokutana na ujumbe kutoka Taasisi isiyo ya Kiserikali ya TYEOO walipomtembelea ofisini kwake jana kwa ajili ya kutambulisha rasmiMradi wa TYEEO Barazani entertainment jana Jini Dar es Salaam.

  Fissoo alisema kuwa mradi huo ni muhimu kwa mustakabari wa kukuza tasni ya Filamu nchini kwani utarahisha kufikisha katika kuwafikia wadau wengi zaidi wa tasni hiyo walioko katika mikoa ya pembezoni.

  “Niseme tu kwa dhati kabisa nawapongeza sana kwa ubunifu wenu mradi huu ni mzuri na utaongeza tija katika tsni yetu ya Filamu, name nina waahidi kuwapa ushirikiano pindi mtakapo kuwa mnahitaji”. Alisema Fissoo.

  Aidha alitoa ushauri kwa Taasisi hiyo kutumia vibanda vya maonyesho ya Filamu vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini ili kutekeleza mradi huo kwa kuwa nia ya Serikali ni kuona dhana ya urathimishaji wa kazi za wasinii inafanikiwa.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TYEEO, John Kallaghe amesema kuwa pamoja na kuwa mradi huo ni binafsi lakini kutokana na imani kubwa waliyonayo juu ya Bodi ya Filamu wameona siyo busara kuendelea kutekeleza jambo kubwa kama hili bila ya kushirikisha mamlaka hiyo ambayo ndiyo msimamizi mkuu wa Tasnia ya Filamu nchini.

  Aliongeza kuwa wazo la kuanzishwa kwa mradi huu ilikuwa ni kusaidia kuwawezesha vijana kujikomboa katika lindi la umaskini kupitia huduma itokanayo na mradi huu ambayo ni utayarishaji na usambazaji wa kazi za wasanii wa Filamu kwa njia ya kisasa zaidi.

  Kallaghe alisema kuwa wao kama wadau tasni hiyo wako tayari kupokea ushauri na maelekezo ya namna ambavyo wanaweza kuboresha na kutekeleza mradi huo kwa ajili ya maendeleo ya taifa kwa ujumla.

  Mradi wa TYEEO Barazani ni miongoni mwa miradi kadhaa ambayo imeanzishwa na taasisi ya TYEEO, ulioasisiwa tangu mwaka 2013 na unakadiriwa kutoa fursa ya ajira za uhakika kwa vijana takribani 6000 katika kada zote za Filamu hadi kufikia mwaka 2017.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Bodi ya Filamu yaahidi ushirikiano uanzishwaji wa Mradi wa TYEEO Barazani Entertainment. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top