728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, September 15, 2016

  ASILIMIA 96 YA WANANCHI WAKUBALI UTENDAJI KAZI WA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI.


  Na Daudi Manongi,MAELEZO.

  Dar es Salaam

  TAKWIMU zilizotolewa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Twaweza imeonyesha kuwa asilimia 96 ya wananchi wanakubali hatua za kiutendaji kazi za Rais John Pombe Magufuli ikiwemo uondoaji wa wafanyakazi hewa na sera ya elimu bure.

  Taarifa iliyotolewa leo katika vyombo vya habari na Mshauri Mwandamizi wa Mawasiliano wa Twaweza, Risha Chande alisema asilimia 88 ya wananchi wana imani kuwa Rais Magufuli ataendelea na kasi aliyoanza nayo mpaka mwisho wa awamu yake ya kwanza ya uongozi.

  “Utafiti huu unaonyesha kuwa asilimia 69 ya wananchi walifuraishwa na juhudi za Rais za uondoaji wa wafanyakazi hewa, wakati asilimia 61 walipongeza sera ya elimu bure wakati asilimia 61 walifurahishwa na usimamishwaji wa watumishi wa serikali” alisema Chande.

  Chande alisema kuwa katika utafiti huo unaonyesha wananchi wengi kuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano ya kufanya maboresho katika huduma za umma ikiwemo mamlaka ya mapat (asilimia 85), mashuleni (asilimia 75),vituo vya polisi (asilimia 74),mahakama (asilimia 73), vituo vya afya (asilimia 72).

  Aliongeza kuwa kwa upande wa huduma zinazotolewa katika utumishi wa umma, utafiti unaonyesha kuwa asilimia 95 ya wananchi wanaridhishwa na huduma zinazotolewa na madaktari, walimu, na maofisa tawala katika ofisi za umma.

  “Pamoja na kiwango kikubwa cha kukubalika kwa Serikali ya wamu ya Tano wananchi wamesema suala la umakini na kanuni za demokrasia na haki ni vyema zifuatwe ambapo wananchi nane kati ya kumi wanasema watendaji waondolewe pale tu panapokuwepo udhibitisho wa vitendo viovu” alisema Chande.

  Akifafanua zaidi Chande alisema utafiti huo pia umeonyesha kubadilika kwa matarajio ya wananchi ambapo katika kipindi cha nyuma kulikuwa na hali ya kutojali miongoni mwa wananchi kulikotokana na utendaji duni kutoka kwa watendaji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: ASILIMIA 96 YA WANANCHI WAKUBALI UTENDAJI KAZI WA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top