728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, August 23, 2016

  ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA AFYA WILAYA YA KASKAZINI ''B'' UNGUJA

  Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar 22/08/2016.

  Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman amesema hapendelei kuona wauguzi wanatumbuliwa majipu kutokana na uzembe wao lakini hayuko tayari kutumbuliwa yeye kwa ajili yao .

  Hayo aliyasema wakati alipokuwa akifanya ziara ya kutembelea vituo mbali mbali vya Afya Wilaya ya Kaskazini B Unguja vikiwemo Kituo cha Kiwengwa na Kituo cha Bubwini Misufini kutaka kuona changamoto zinazopo vituo hapo.

  Alisema kuna baadhi ya wauguzi huwafanyia dharau wagonjwa au wajawazito wakati wa kujifungua jambo ambalo halipaswi kuona linafanyika, kitu ambacho kinaweza kuwapeleka pabaya na kutumbuliwa majibu.

  “Sitoona vizuri kuona mfanyakazi anatumbuliwa jipu kwa ajili ya uzembe wake na pia siko tayari kutumbuliwa mimi kwa ajili yake “Alisema Harusi .

  Aidha alisema kwamba wauguzi wawetayari kukamilisha majukumu yao ya kikazi na waache lugha chafu ambazo zitawasumbuwa wagonjwa na kuonekana kuwa wao wakorofu katika kutoa huduma .

  Hata hivyo Naibu Waziri alieleza kuwa wauguzi waelewe kuwa awamu iliopo hivi sasa ni awamu ya uwajibikaji na ufatiliaji na ni rahisi mawasiliano kufika kwa haraka na kuweza kuharibu malengo ya baadae hivyo wasiwe tayari kuchokozwa wakachokozeka.

  Nae Muuguzi wa kituo cha afya cha Kiwengwa Khadija Ali Juma alieleza matatizo mbali mbali ambayo wanakabiliana nayo kituoni hapo ikiwemo kutokuwa na uzio katika eneo hilo, wananchi kuchafua katika kwa makusudi katika maeneo ya vyoo pamoja na kufanya maskani katika kituo hicho .

  Aidha alisema kutokuwa na friji katika kituo hicho kunachagia usumbufu mkubwa wa kuhifadhia dawa za chanjo za mama na watoto ambazo zinahitajika kuhifadhiwa katika sehemu yenye ubaridi ili zisiharibike .

  Alisema ushirikiano mdogo uliopo baina ya kituo cha afya na kamati ya sheha hawaufurahikii wauguzi ,kwani sheha wa sehemu hiyo haonyeshi ushirikiano mzuri na wauguzi waliopo katika kituo hicho .

  Wakati huo huo Naibu Waziri wa Afya alitembelea katika Kituo cha Afya cha Bumbuni Misufini ambacho kilitokezea matatizo ya kutofahamiana kati ya Wauguzi wa serikali na Wakunga wa Jadi .

  aliwataka wauguzi ambao ni waajiriwa wa serikali kutoa mashirikiano ya pamoja na wakunga wa jadi ili kuepusha tofauti miongoni mwao na kuweza kutatua changamoto ambazo zitaweza kujitokeza kwa wazazi .
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA AFYA WILAYA YA KASKAZINI ''B'' UNGUJA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top