728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, August 13, 2016

  YANGA YAIKUNA 1-0,YAJIPA MATUMAINI MAKUBWA YA KUIBAMIZA TP MAZEMBE  Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva akiachia shuti la hatari kwa kipa wa Bejaia  . Yanga wameibuka kidede kwa goli 1-0 dhidi ya Bejaia
   Golikipa wa Yanga akiokoa mpira wa hatari uliokuwa ukitinga nyavuni kwake
   Mshambuliaji wa timu ya Yanga Simon Msuva akikokota mpira kuelekea lango la Bejaia.
  kipa wa Bejaia akiokoa moja ya hatari iliyoelekezwa langoni mwake na Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva. Yanga wameibuka kidede kwa goli 1-0 dhidi ya Bejaia.

  BAADA ya Kupata ushindi wa kwanza walioupata Yanga, Koch mkuu wa Hans Van De Pluijm amesema ushindi huu umempa nguvu katika kuelekea mchezo unaofuata dhidi ya TP Mazembe.

  Yanga imefanikiwa kushinda goli 1-0  lililofungwa na Mchezaji wa kimataifa kutoka Zimbabwe Thaban Kamosoku dakika ya tatu dhidi ya Mo bejaia mechi iliyofanyika kwenye dimba la uwanja wa Taifa.

  Pluijm amesema kuwa, wachezaji wake wamecheza vizuri sana na wameweza kulinda goli katila dakika zote ingawa kuna makosa madogo madogo yaliyojitokeza ila anawapa hongera kwa jitihada walizozifanya.

  Naye Nahondha wa Yanga, Vicent Bossou amesema wamefanya kazi kubwa sana katika kuhakikisha wanatoka ushindi na wamecheza timu nzuri sana yenye uzoefu wa muda mrefu wa michuano ya kimataifa ila anawapongeza pia wachezaji wenzake kwa jitihada walizozifanya.

  Baada ya ushindi huo Yanga wanaendea kusalia katika nafasi ya nne wakiwa na alama nne huku mchezo kati ya Mazembe na Medeama ukitarajiw kuchezwa kesho nchini Ghana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: YANGA YAIKUNA 1-0,YAJIPA MATUMAINI MAKUBWA YA KUIBAMIZA TP MAZEMBE Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top