JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WIZARA YA AFYA YATOA UFAFANUZI UPUNGUFU WA CHANJO YA KICHAA CHA MBWA NA HOMA YA MANJANO.

Share This

 Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara hiyo Dk. Neema Rusimabayila akitoa ufafanuzi kuhusu Chanjo ya Homa ya Manjano na vitendo vya baadhi ya watumishi wa afya   wasiowaaminifu  ambao hulipwa fedha ili waweze kuwatengenezea wasafiri kadi za Chanjo ya Homa ya Manjano na kisha kuzitumia nje ya nchi jambo ambalo kinyume cha sheria  na hatari kwa usalama wa Afya zao.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mohamed Mohamed akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya hatua iliyochukuliwa na Serikali kuagiza na kusambaza dozi mbalimbali za chanjo kupitia mpango Serikali wa kukabiliana na changamoto ya upungufu wa chanjo uliojitokeza nchini.
 Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dafrosa Lyimo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu mpango wa utoaji wa chanjo  zilizokuwa na upungufu zikiwemo za kifua Kikuu, Polio, Surua na Lubela ambazo MSD wamekwisaha anza kuzisambaza.

Na. Aron Msigwa – Dar es salaam.
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) inatarajia kupokea dozi 14,000 za chanjo ya homa ya manjano mwanzoni mwa mwezi Septemba, 2016 ili kutosheleza mahitaji ya wasafiri watakaohitaji huduma hiyo kwa kipindi cha mwaka mzima.

Aidha, Wizara hiyo imekwisha nunua dozi za chanjo ya Kifua Kikuu na Polio 739,700 na kusambaza dozi zipatazo milioni  7 kwenye mikoa ya Morogoro, Singida, Dodoma, Tabora na Kigoma.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mohamed Mohamed amesema kuwa uagizaji na usambazaji wa dozi hizo ni mpango Serikali wa kukabiliana na changamoto ya upungufu wa chanjo uliojitokeza nchini.

Akifafanua kuhusu kukosekana kwa baadhi ya chanjo ikiwemo ya Homa ya Manjano amesema hali hiyo imetokana na kutokea kwa mlipuko wa homa hiyo katika nchi za jirani ikiwemo Angola jambo lililosababisha akiba ya chanjo hiyo dunia nzima kupelekwa kwenye nchi zenye mlipuko wa ugonjwa huo kwa lengo la kuwachanja wananchi wote ili kuzuia ugonjwa huo kusambaa.

Amesema kutokana na hali hiyo akiba iliyokuwa imewekwa kwa ajili ya kuzigawia nchi nyingine hasa matumizi kwa ajili ya wasafiri ilibidi ipelekwe katika maeneo yaliyokuwa na upungufu wa dozi hizo kutokana na uharaka na uhitaji wa chanjo hizo.

Amesema wizara kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) inatekeleza mradi wa majaribio wa kutokomeza kichaa cha mbwa kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara, Morogoro, Pwani na Dar es salaam ambayo sasa ina chanjo za kichaa cha mbwa.

Amebainisha kuwa jijini Dar es salaam chanjo hizo zinapatikana katika hospitali ya wilaya ya Temeke, Kituo cha Afya Magomeni.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara hiyo Dk. Neema Rusimabayila akitoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya watoto waliokosa chanjo katika awamu tofauti amesema kuwa wote waliokosa chanjo kuhakikisha kuwa wanamaliza chanjo zao kwa mujibu wa idadi ya chanjo walizopangiwa pindi zitakapopatikana.

Ametoa wito kwa wataalam wa afya wanaohusika na utoaji wa chanjo kuwapatia taarifa wazazi wenye watoto ambao walihudhuria vituo vya afya kisha kukosa chanjo hizo, kuhakikisha kuwa wanarudi katika vituo vya afya ili waweze kumalizia idadi ya chanjo walizotakiwa kupata pindi zitakapofikishwa kwenye vituo vyao.

 Kuhusu Mradi wa majaribio wa kipindi cha miaka 5 wa chanjo ya kichaa cha mbwa wenye lengo la kuondoa kichaa cha mbwa amesema kuwa unalenga kupunguza idadi ya wagonjwa na vifo vya watu vinavyotokana na kichaa cha mbwa.

Naye Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo wa Wizara hiyo Dk. Dafrosa Lyimo akifafanua kuhusu mpango wa utoaji wa chanjo  zilizokuwa na upungufu hizo amesema kuwa mpaka sasa utaratibu wa kupokea chanjo zaidi  zikiwemo za kifua` Kikuu, Polio, Surua na Lubela ambapo MSD wamekwisaha anza kuzisambaza.

Ametoa wito kwa wazazi wenye watoto waliokosa chanjo kuwasiliana na vituo husika ili waweze kupangiwa ratiba ya kupatiwa chanjo hizo kwenye vituo vya kutolea huduma vya serikali ndani ya umri wa miaka 5.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad