728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, August 11, 2016

  WATANZANIA ZAIDI YA 1000 WANUFAIKA NA MAFUNZO NCHINI JAPANI


  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza katika hafla fupi ya kuwaaga watumishi waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative, iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini mapema leo
  Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Masaharu YOSHIDA akizungumza katika hafla fupi ya kuwaaga watumishi waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative, iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini mapema leo.
  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi (12)waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative awamu ya tatu (03), mara baada ya hafla fupi ya kuwaaga watumishi hao iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini mapema leo.
  Watumishi (12) waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative awamu ya tatu (waliosimama) wakijitambulisha mbele ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro ( wa pili kulia mstari wa mbele) na Waandishi wa Habari (kushoto) wakati wa kipindi cha maswali na majibu mara baada ya hafla fupi ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi hao iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini mapema leo.
  Mwandishi wa habari wa gazeti la Dailynews Bi. Hilda Mhagama (wa kwanza kushoto) akiuliza swali kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro( wa pili kulia mstari wa mbele) wakati wa kipindi cha maswali na majibu mara baada ya hafla fupi ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi hao iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini mapema leo.
  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro( wa pili kulia mstari wa mbele) akijibu swali aliloulizwa na Mwandishi wa habari wa gazeti la Dailynews Bi. Hilda Mhagama (wa kwanza kushoto) wakati wa kipindi cha maswali na majibu mara baada ya hafla fupi ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative awamu ya tatu, iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini mapema leo.

  Mahusiano yaliyodumu kwa muda mrefu baina ya Serikali ya Tanzania na Japani yamewezesha watanzania zaidi ya 1000 kupata mafunzo katika vyuo mbalimbali nchini Japani kwa kipindi cha miaka 8 ambayo yamesaidia kuwa na rasilimaliwatu yenye tija katika maendeleo ya kiuchumi nchini Tanzania.

  Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menentimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro kwenye hafla fupi ya kuwaaga watanzania 12 waliopata fursa ya mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani kwa ufadhili Serikali ya Japani kupitia Mpango wa ABE initiative, iliyofanyika leo nyumbani kwa balozi wa Japani nchini Tanzania .

  “ Kati ya mwaka 2008 hadi 2015 zaidi ya watanzania 1000 wamepata mafunzo katika vyuo mbalimbali nchini Japani kupitia ufadhili wa Shirika la kimataifa la Maendeleo la Japani ( JICA) na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuwajengea uwezo watumishi wa umma na watumishi walio katika sekta binafsi” alisema Dkt. Laurean Ndumbaro.

  Dkt. Ndumbaro alifafanua kuwa, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Maendelo la Japani limewawezesha vijana wengi wa kitanzania kupata mafunzo ya shahada ya Uzamili kupitia Mpango wa ABE initiative,ambao baada ya kumaliza mafunzo , wanarudi nchini Tanzania na kuanza kujenga ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Japani na pia kuchangia katika maendeleo ya sekta ya viwanda nchini” alisisitiza Dkt. Ndumbaro

  “ Katika awamu ya kwanza mwaka 2014 walienda vijana 29 na awamu ya pili ambayo ni mwaka 2015 walienda vijana 32 kwa ajiri ya kupata mafunzo nchini Japani, ambapo mpaka sasa idadi ya wanufaika wa mafunzo hayo imefikia 73” alifafanua Dkt. Ndumbaro. Aidha Dkt. Ndumbaro aliwataka vijana waliopata fursa ya mafunzo hayo nchini Japani kusoma kwa bidii na kutumia elimu na ujuzi watakaoupata kuleta maendeleo ya kiuchumi nchini.

  Alisema, ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na Japani umeanza tangu mwaka 1960 ambapo kwa mara ya kwanza Tanzania ilipata fursa ya kupeleka watanzania nchini Japani mwaka 1962 kwa ajili ya kupata mafunzo katika vyuo mbali mbali nchini humo. Kwa upande wake Balozi wa Japani nchini Mhe. Masaharu Yoshida alisema, Japan itaendelea kudumisha ushirikiano wa muda mrefu uliopo baina ya nchi hizo mbili ili kila upande unufaike kupitia ushirikiano huo.

  Naye Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani nchini (JICA) Bw. Toshie Nagase amesema, vijana 12 waliopata nafasi ya mafunzo nchini Japani kupitia Mpango wa ABE initiative ni kati ya 52 walioomba nafasi hiyo, hivyo hawanabudi kuitumia fursa hiyo kujifunza kwa bidii kwa ajili ya manufaa ya nchi.

  Mpango wa ABE initiative wa miaka 5 ulianzishwa nchini Japani mwaka 2013 na Waziri Mkuu wa Japani Mhe. Shinzo ABE ambaye alitambua umuhimu wa kusaidia uwezeshaji wa maendeleo endelevu ya kiuchumi barani Afrika, mpango huo ulilenga kunufaisha vijana 1000 wa kiafrika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WATANZANIA ZAIDI YA 1000 WANUFAIKA NA MAFUNZO NCHINI JAPANI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top