728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, August 3, 2016

  Wananchi Zanzibar watakiwa kulipia huduma ya maji

  Na Rahma Khamis Maelezo -Zanzibar

  Wananchi wa Zanzibar wametakiwa kulipia huduma ya maji kwa wakati ili kuweza kupata huduma hiyo kwa ufanisi zaidi na kuepukana na usumbufu unaoweza kujitokeza.

  Wito huo umetolewa na Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Zahour Suleiman Ofisini kwake Msikiti Mabuluu Mjini Zanzibar wakati akitoa maelezo kuhusiana na ulipaji wa huduma ya maji.

  Amesema maji ni moja ya huduma muhimu katika maisha ya wananchi hivyo ni muhimu kuhakikisha yanapatikana muda wote na suala la kulipia huduma hiyo ili iwe endelevu ni jambo la msingi.

  Afisa huyo amefahamisha kuwa badhi ya wananchi wamekuwa na mwamko mdogo katika kulipia huduma ya maji na kusababisha Mamlaka kukosa uwezo wa kutoa huduma hiyo kwa ufanisi.

  Aidha amesema kuwa kwa sasa huduma hiyo inaelekea kuzidiwa kutokana na kukuwa kwa harakati za kimaendeleo hasa kwa matumizi ya kilimo ambacho kinatumia maji mengi ukilinganisha na matumizi ya majumbani.

  Afisa huyo amefahamisha kuwa wameanzisha utaratibu wa kupita katika maeneo kwa lengo la kutoa elimu kuhusiana na umuhimu wa kulipia maji na wale watakaoshindwa kuufahamu mpango huo Mamlaka huwapa onyo na baadae kusitishwa kupata huduma.

  Sambamba na hayo Zahour amewashauri wanajamii kufuata sheria bila ya kushurutishwa kwa kulipia maji kwa wakati ili kuipa uwezo Mmlaka ya maji kutekeleza wajibu wake wa kuwapatia wananchi huduma hiyo kama kawaida.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Wananchi Zanzibar watakiwa kulipia huduma ya maji Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top