728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, August 30, 2016

  WANAFUNZI WA CHUO CHA DIPLOMASIA WAMNUNULIA MWENZAO VIFAA VYA KUMSAIDIA KUSIKIA


  Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Diplomasia Dk Bernald Achiula akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo wakati akishukuru wanafunzi wa chuo hicho kwa michango yao waliyochanga ili kumsaidia mwanafuzni mwenzao Shinuna Salum Nyamkokwa ambaye ana matatizo ya kusikia, wanafunzi hao wamechanga Fedha na kumnunulia mwenzao Vifaa vya kumsaidia kusikia vyenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano, Kulia ni Mwanafuzni Shinuna Salum Nyamkokwa ambaye ameelezewa kuwa ana uwezo mkubwa katika masomo yake darasani pamoja na kutokuwa na uwezo wa kusikia, na Katikati ni Neema Zawadi Henjewele Makamu wa Rais Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia.
  Neema Zawadi Henjewele Makamu wa Rais Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia akielezea kwa waandishi wa habari kuwa kitu kilichowafanya wanafunzi wa chuo hicho kumchangia mwanafunzi mwenzao Shinuna Salum Kulia ni kutokana na uwezo wake katika masomo pamoja kuwa tatizo la usikivu linalomkabili
  Mwanafuzni huyo Shinuna Salum Nyamkokwa akizungumza mbele ya waandishi wa habari wakati akielezea kuhusu msaada wa vifaa hivyo ambapo amesema awali kichwa kilikuwa kinamuuma sana lakini kwa sasa hakiumi tena.
  Gordian Kilave Mkuu wa Idara ya Lugha Chuo cha Diplomasia akielezea matatizo yaliyokuwa yakimkuba na kumsumbua mwanafunzi Shinuna Salum kabla ya kupatiwa vifaa hivyo ambavyo ninamsaidia kusikia kwa sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WANAFUNZI WA CHUO CHA DIPLOMASIA WAMNUNULIA MWENZAO VIFAA VYA KUMSAIDIA KUSIKIA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top