728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, August 7, 2016

  WAKAZI WA MANISPAA YA KINONDONI TAARIFA HII NI FEKI,IPUUZENI.


  Wakazi wa manispaa ya kinondoni.

  Kuna karatasi linazunguka mitaani kuwa ni sheria mpya za halmashauri ya manispaa ya kinondoni, likionyesha tozo mbalimbali za uegeshaji magari kando ta barabara na gharama zake.

  Hiyo nyaraka si nyaraka halali wala rasmi ya manispaa ya kinondoni;

  • Haina afisa muidhinishaji, Kwa niaba au mkurugenzi na saini yake,pamoja na terehe ya kutolewa.

  •Hakuna mkataba mpaka sasa ulioingiwa na manispaa wala kikao kilicho kaa kupitisha jambo hilo.

  Tunawaomba mpuuzie na msiwe na hofu na jambo hilo kwa maana sio halali mpaka mtakapo julishwa rasmi kama lipo.

  Watu wenye nia ovu na taswira ya manispaa ya kinondoni huenda wana ajenda wanayoijua, bali si mamlaka halali.

  Mstahiki Meya, Manispaa ya Kinondoni
  Boniface Jacob
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAKAZI WA MANISPAA YA KINONDONI TAARIFA HII NI FEKI,IPUUZENI. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top