728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, August 21, 2016

  UWT NA CCM MUFINDI WAMPONGEZA RAIS DR MAGUFULI


  Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mufindi Bi Marcelina Mkini akizungumza katika kikao cha baraza la wanawake wilaya ya Mufindi hivi karibuni


  Na MatukiodaimaBlog

  UMOJA wa wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa umempongeza Rais Dr John Magufuli kwa utendaji kazi mzuri wenye lengo la kuwakomboa watanzania hasa wanyonge huku ukiwataka viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kuwa na huruma na watanzania .

  Washauri CHADEMA kuachana na harakati zao za umoja wa kupinga udikteta Tanzania (UKUTA) Kuwa harakati hizo si za kimaendeleo bali ni harakati zenye lengo la kuchafua sifa ya kazi inayofanywa na serikali ya Rais Dr Magufuli jambo ambalo si la kulifumbia macho .

  Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mufindi Bi Marcelina Mkini alisema hayo leo mbele ya wanahabari wakati akitoa pongezi zake kwa Rais Dr Magufuli kukabidhiwa mikoba ya uenyekiti wa CCM Taifa na jinsi alivyoleta matumaini kwa wananchi kutokana na zoezi la kutumbua majipu ,alisema hivi sasa wana CCM wanatembea kifua mbele tofauti na awali ambapo sifa ya fisadi ilionekana kuwanyima raha wana CCM.

  Bi Mkini alisema kuwa UWT Mufindi inampongeza Rais Dr Magufuli kwa kuonyesha utendaji kazi wa vitendo zaidi na hivyo kupelekea Taifa la Tanzania kuendelea kuwa moja kati ya mataifa ya mfano kwa kuwa na Rais bora mchapakazi.

  Hata hivyo alisema wao kama UWT hawaungi mkono wala hawapendezwi na siasa chafu zinazopangwa kufanywa na CHADEMA kwa kisingizio cha kupinga udikteta Tanzani jambo ambalo halipo na kuwa wanaopinga kasi ya Rais katika kuwatumikia wananchi na kutaka watu wafanye maandamano yasiyo na tija wao ni madikiteta ila watanzania wapenda maendeleo anachokifanya Rais Dr Magufuli ni ukombozi kwao.

  “ Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wetu mpendwa Dr John Magufuli ni serikali ya kazi na vitendo zaidi kwa ajili ya kuwasaidia watanzania kupiga hatua ya kimaendeleo na ni vema kutambua kuwa uchaguzi mkuu ulimalizika mwaka jana na sasa si wakati wa kampeni za kuchafuana ni wakati wa kila mmoja kuwatumikia wananchi …..sasa ukiona chama kinalazimisha maandamano kwa sasa ni kukosa kazi ya kufanya na huo ni zaidi ya udikteta lazima viongozi wa vyama vya siasa kuwa na huruma kwa watanzania badala ya kuwatumikisha maandamano yasiyo na faida kwao”

  Aliwataka wanawake wote wilayani Mufindi kuwazuia vijana wao kujishughulisha na maandamano hayo ya UKUTA na badala yake kuwapa elimu ya kujiunga na vikundi vya ujasiliama mali ikiwa ni pamoja na kuvisajili ili kuweza kunufaika na mpango mzuri wa Rais Dr Magufuli wa kutoa fedha kiasi cha Tsh milioni 50 kwa kila kijiji .

  Pia alisema wao UWT Mufindi kwa kuunga mkono kazi nzuri ya Rais wataendelea kuhamasisha wanawake kujiunga na vikundi vya kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuonyesha mfano kwa wilaya nyingine.

  Kuhusu zoezi la kutumbua majipu na wafanyakazi hewa alisema zoezi hilo linapaswa kuendelea zaidi na kuwa Rais ni mwenyekiti wa chama Taifa bado wanaomba muda ukifika wa kutumbua majipu ndani ya CCM asiache kufanya hivyo kwani sifa ya chama imekuwa ikichafuliwa na viongozi wachache ambao kama mwenyekiti mwenyewe wa Taifa alivyosema kuwa wapo wanaohujumu chama wakiwa ndani ya chama .
  Katibu wa CCM wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama akisoma taarifa ya wilaya hiyo kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi (kulia). katikati ni Mwenyekiti wa wilaya ya mufindi Bw Kaguo

  .Katibu wa CCM wilaya ya Mufindi Bw Jimson Mhagama pamoja na kumshukuru Rais kwa kuzuia maandamano ya UKUTA alisema kuwa haoni faida ya maandamano hayo hivyokuwaomba wananchi wa Mufindi kuelekeza nguvu zao katika shughuli za maana na kuachana na maandamano hayo na kama yapo basi viongozi wa Chadema na familia zao ndio waandamane na si vinginevyo ili kama kupigwa na kukamatwa basi wakamatwe wao ambao wananufaika na maandamano hayo .
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: UWT NA CCM MUFINDI WAMPONGEZA RAIS DR MAGUFULI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top