728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, August 22, 2016

  UTOAJI WA MALALAMIKO NA KERO JUU YA HUDUMA ZA AFYA NCHINI PAMOJA NA MASUALA YA JINSIA, WAZEE NA WATOTO


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO


  UTOAJI WA MALALAMIKO NA KERO JUU YA HUDUMA ZA AFYA NCHINI PAMOJA NA MASUALA YA JINSIA, WAZEE NA WATOTO

  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inayo dhamana ya kusimamia na kuratibu Mipango, Sera, Sheria na Mikakati mbalimbali inayolenga kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini pamoja na kujenga jamii ya watanzania inayojali na kuheshimu Usawa wa Jinsia, Haki za Wazee na Watoto.

  Katika utekelezaji huu, yapo mafanikio kadhaa yaliyopatikana lakini pia zipo changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utoaji wa huduma za afya hapa nchini. Baadhi ya changomoto hizo ni za kiutendaji zaidi ambazo zinaweza kutatuliwa kwa haraka endapo tutaimarisha usimamizi na uwajibikaji katika kila ngazi kuanzia ngazi ya Wizara, Mikoa, Wilaya na Vituo vya kutolea huduma za afya. 

  Changamoto hizi ni pamoja na wagonjwa kutopatiwa huduma haraka na sahihi, lugha na kauli mbaya kutoka kwa watoa huduma na makundi yanayotakiwa kupata matibabu bure (yaani Wazee, Wajawazito na Watoto wa umri wa chini ya miaka 5) kutozwa fedha kinyume na Sera ya Afya ya 2007). Takribani kila siku vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti matukio kadhaa kuhusu malalamiko na kero mbalimbali wanazokumbana nazo wananchi  katika kupata huduma za afya.

  Wasimamizi wa Wakuu wa Utekelezaji wa Sera na Miongozo ya Afya katika ngazi ya Mikoa ni Waganga Wakuu wa Mikoa. Ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya pamoja na kuhakikisha malalamiko na kero zao zinashughuhulikiwa kwa haraka, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) ameamua kuweka wazi namba za simu za Waganga Wakuu wa Mikoa (RMO) wote nchini ili wananchi wanapokuwa na malalamiko/kero waweze kuwasiliana nao moja kwa moja. 

  Mhe Waziri amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa kuyafanyia kazi masuala yote yanayoletwa na wananchi katika Mikoa yao na kuyapatia ufumbuzi haraka. Hivyo, wananchi wasisite kuwasiliana nao kupitia namba zao zifuatazo pamoja na kwa barua pepe.

  Katika muktadha mzima wa kuongeza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa Sheria na Sera za Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini, mwananchi yoyote ambae ana malalamiko, maoni au ushauri kuhusu sekta husika unaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mheshimiwa Waziri, Ummy Mwalimu (Mb) kupitia simu namba 0746 – 505030 (kwa njia ya ujumbe) pamoja na kueleza mkoa uliopo, twitter @wamjw na email: waziri@moh.go.tz

  “Uwazi na Uwajibikaji ni chachu ya kuleta mabadiliko katika sekta ya afya, sambamba na kulinda Haki za Watoto, Wazee na Wanawake”.  MAWASILIANO NA WAGANGA WAKUU WA MIKOA (RMOs)

  NA.
  MKOA
  JINA LA MGANGA MKUU
  NAMBA YA SIMU
  NUKUSHI
  1.
  ARUSHA
  DKT. FRIDA MOKITI
  0784-264750
  fridamokiti@yahoo.com.
  2.
  DAR ES SALAAM
  DKT. GRACE MAGEMBE
  0767-300234
  magembegrace@yahoo.com
  3.
  DODOMA
  DKT. JAMES CHALRES
  0784-504955
  jcrexford@yahoo.com
  4.
  IRINGA
  DKT. ROBERT M. SALIM
  0754-377176
  saludimwe@yahoo.com
  5.
  KAGERA
  DKT. THOMAS RUTACHUNZIBWA
  0754-803729
  thomasruta@yahoo.com
  6.
  KIGOMA
  DKT. PAUL CHAOTE
  0755-696855
  pchaote@gmail.com
  7.
  KILIMANJARO
  DKT. BEST MAGOMA
  0754-621046

  8.
  LINDI
  DKT. SONDA YUSUPH
  0653-384350
  sonda_y@yahoo.com
  9.
  MANYARA
  DKT. SUNGWA KABISSI NDAGABWENE
  0713-450765
  Mas19730ok@yahoo.co.uk
  10.
  MARA
  DKT. SAMSON WINANI
  0784-450425
  sam.winani@yahoo.co.uk
  11.
  MBEYA
  DKT. SEIF MHINA
  0767-832275
  sbmhina@gmail.com
  12.
  MOROGORO
  DKT. JACOB FRANK
  0767-985850

  13.
  MTWARA
  DKT. WEDSON SICHALWE
  0755-048787

  14.
  MWANZA
  DKT. LEONARD SUBI
  0784-501020
  subileon@yahoo.com
  15.
  PWANI
  DKT. BEATRICE BYARUGABA
  0784-319764
  bykami@yahoo.com
  16.
  RUKWA
  DKT. JOHN GURISHA
  0784-216008
  igurisha@yahoo.com
  17.
  RUVUMA
  DKT. DAMAS KAYERA
  0713-537495
  dajkay@gmail.com
  18.
  SHINYANGA
  DKT. NTULI KAPOLOGWE
  0654-586346
  nkapologwe2002@gmail.com
  19.
  SIMIYU
  DKT. MAGEDA KIHULYA
  0754-507875
  mkihulya@yahoo.com
  20.
  SINGIDA
  DKT. JOHN MWOMBEKI
  0786-103225
  johnmwombeki@yahoo.co.uk
  21.
  TABORA
  DKT. GUNINI KAMBA
  0783-344079
  gunini@yahoo.com
  22.
  TANGA
  DKT. ASHA MAHITA
  0715-465521
  ashamahita@yahoo.co.uk
  23.
  GEITA
  DKT. JOSEPH KISALA
  0788-046787
  joskisala@gmail.com
  24.
  KATAVI
  DKT. YAHYA HUSSEIN
  0754-372772
  hyahaya70yahoo.com
  25.
  NJOMBE
  DKT. SAMUEL MGEMA
  0757-226806
  mgemasamuel@gmail.com

  IMETOLEWA TAREHE 22/08/2016
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: UTOAJI WA MALALAMIKO NA KERO JUU YA HUDUMA ZA AFYA NCHINI PAMOJA NA MASUALA YA JINSIA, WAZEE NA WATOTO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top