728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, August 10, 2016

  UDART NA MAXMALIPO ZAINGIA MKATABA WA PAMOJA


  Msemaji wa Kampuni ya Mabasi ya Mwendo wa haraka jijini Dar es Salaam (kushoto) Bw. Deus Bugaywa akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kuweka salio katika kadi za mabasi ya mwendo wa haraka kupitia kwa mawakala wa MaxMalipo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, Katikati ni Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Maxcom Africa Ltd. Bw. Ahmed Lussasi na mwisho kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara toka Maxmalipo Bw. Deogratius Lazari.
  Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Maxcom Africa Ltd. Bw. Ahmed Lussasi akionesha moja ya kadi za mabasi ya mwendo wa haraka wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kuweka salio katika kadi za mabasi ya mwendo wa haraka kupitia kwa mawakala wa MaxMalipo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Msemaji wa Kampuni ya Mabasi ya Mwendo wa haraka jijini Dar es Salaam (kushoto) Bw. Deus Bugaywa
  Mkuu wa Kitengo cha Biashara toka Maxmalipo Bw. Deogratius Lazari akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) namna ya kufanya malipo wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kuweka salio katika kadi za mabasi ya mwendo wa haraka kupitia kwa mawakala wa MaxMalipo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Maxcom Africa Ltd. Bw. Ahmed Lussasi.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimfuatilia kwa makini Mkuu wa Kitengo cha Biashara toka Maxmalipo Bw. Deogratius Lazari namna ya kuongeza salio kwenye kadi za mabasi ya mwendo wa haraka wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kuweka salio katika kadi za mabasi ya mwendo wa haraka kupitia kwa mawakala wa MaxMalipo mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Eliphace Marwa - Maelezo.

   


  DART na MAXCOM wazindua mfumo wa kuweka salio katika kadi za mabasi ya mwendo wa haraka kupitia mawakala wa Maxmalipo.


  Na Eliphace Marwa -Maelezo

  Kampuni ya Maxcom Africa – Maxmalipo kwa kushirikiana na Kampuni ya Mabasi yaendayo Haraka wamezindua rasmi Mfumo unaowezesha watumiaji wa Usafiri wa Mwendo haraka (mwendo Kasi) kuweka salio katika kadi za usafiri kupitia kwa Mawakala wa Maxmalipo popote hapa nchini.

  Hivyo kuanzia sasa wasafiri wenye kadi maalumu za Usafiri (Dart card) wanaweza kufika kwa wakala yeyote wa Maxmalipo kisha atampatia fedha taslimu yenye thamani na salio analohitaji kuweka ndani ya kadi yake na Wakala atamukea salio ambalo litamwezesha kusafiri katika mabasi ya mwendo haraka kwa kutumia kadi yake hiyo.

  Akiongea kwenye uzinduzi huu Afisa Mwendesgaji mkuu wa Maxmalipo Bw. Ahmed Lussasi Amesema kuwa kampuni ya Maxcom imekuwa msatari wa mbele katia kujenga mifumo imara ya kieletroniki inayorahisisha ukusanyaji wa mapoato.

  “ Lengo kubwa la kampuni ya Maxcom Africa ni kujenga na kutengeneza mifumo imara na madhubuti ambayo inalenga kurahisisha ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki pia kusimamia na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato kwa kutumia mifumo ya Kielektroniki,” alisema Bw. Lussasi.

  Naye Msemaji wa Kampuni ya Mabasi yaendayo Haraka Bw. Deus Bugaywa aliongeza kuwa Maxmalipo ikishirikiana na Uongozi wa mradi wa mabasi ya mwendo haraka wamekua mstari wa mbele katika kufanya uvumbuzi wa njia mbalimbali za kiteknolojia zitakazo warahisishia wasafiri pamoja na watumiaji wa mabasi haya kuendelea kujipatia huduma kwa urahisi zaidi bila usumbufu wowote.

  “Naweza kuwadhihirishia kwa ushirikiano huu tulionao na Maxmalipo katika mradi huu umeleta mageuzi makubwa katika sekta ya usafirishaji nchini kwetu, barani Afrika na duniani kwa ujumla,” alisema Bw. Bugaywa.

  Naye Mkuu wa Kitengo cha biashara katika kampuni ya Maxmalipo Bw. Deogratius Lazari, amesema kuwa Maxcom Africa ina Zaidi ya mawakala 15000 nchi nzima ambao wamewezeshwa kutoa huduma hii kwa watumiaji wa kadi hizi za mwendo haraka.

  “Mawakala hawa wa Maxmalipo wapo jirani na makazi ya watu hivyo wasafiri wanaweza kujipatia huduma hii kabla ya kufika kwenye vituo vya mabasi ya mwendo haraka na kupunguza foleni za abiria kwenye vituo vya mabasi ya hasa wale wanaokua wakihitaji kuweka salio kwenye kadi zao,” alisema Bw. Lazari.

  Maxcom Africa imekua ni Moja ya Kampuni za Kitanzania iliyofanikiwa katika uwekaji wa mifumo madhubuti ya ukusanyaji na usimamizi wa mapato hapa Tanzania hasa katika miradi mikubwa ikiwamo huu wa mabasi ya Mwendo Kasi, TRA, Vivuko, Mahospitali (Moi) na kwenye Kodi za halmashauri.

  MWISHO.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: UDART NA MAXMALIPO ZAINGIA MKATABA WA PAMOJA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top