728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, August 5, 2016

  TUMEKATA RUFAA ILI KUPATA MAAMUZI KUTOKA CHOMBO CHA JUU YATAKAYOKUWA KAMA SHERIA


  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea vitabu na vipeperushi mbalimbali kutoka kwa mjumbe wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) baada ya kumaliza mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe katika ukumbi wa mikutano wa Wizara jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akipokea vitabu na vipeperushi mbalimbali kutoka kwa mjumbe wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) baada ya mkutano na Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe katika ukumbi wa mikutano wa Wizara jijini Dar es salaam.  Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) Bi. Anastazia Soka (mwenye miwani) akiongea katika ukumbi wa mikutano ghorofa ya Nane wakati wa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe jijini Dar es Salaam.  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria akiongea na wanawake wa Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA) walipomtembelea kubadilishana mawazo mbalimbali kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria hasa kwa upande wa Wanawake katika Ukumbi wa mikutano ghorofa ya Nane jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria.


  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe amesema Serikali imeamua kukata rufaa Mahakama ya Rufani dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu uliosema kipengele cha umri wa mtoto wa kike kuolewa kinakiuka Katiba ili kuweza kupata maamuzi ya chombo cha juu cha Mahakama ambayo hayatweza badilishwa na hivyo kuwa kama Sheria .

  Amesema sio kama Serikali inapingana na uamuzi wa Mahakama Kuu, ila kinachofanyika ni utaratibu wa kawaida ambao utaiwezesha Serikaki kuwa na maamuzi kutoka katika Chombo cha Juu Kabisa cha Mahakama nchini na hivyo maamuzi hayo hayataweza kutenguliwa na mtu au chombo chochote na kuongeza kuwa ukibaki uamuzi huo pekee inaweza ikatokea siku nyingine Jaji mwingine akatoa maamuzi tofauti na hayo.

  “Jamani , nimesikia mengi, Sio kama Serikali inapingana na uamuzi wa Mahakama Kuu, ila kinachofanyika ni sasa ni utaratibu wa kawaida ambao utaiwezesha Serikali kupata maamuzi kutoka katika Chombo cha Juu Kabisa cha Mahakama nchini, maamuzi hayo yakitolewa hakutakuwa na mtu au chombo kingine kitakachokuwa na mamlaka ya kutoa maamuzi mengine juu ya suala hilo alisema na kuongeza kuwa tumefanya hivyo ili Mahakama ya Juu kabisa ithibitishe juu ya suala hilo ili ijulikane moja, alisema Dkt Mwakyembe.

  Amewasihi wanasheria wanawake na wanaharakati wengine wanaoshughulikia haki za wanawake na watoto nchini kufahamu kuwa Serikali ina nia njema na inaliona suala la mtoto kuolewa kabla ya kufikisha miaka 18 kama miongoni mwa changamoto nyingi inazozikabiliana nazo na ndio maana hata ikapitisha sheria inayosema atakayemuoa mwanafunzi atachukuliwa hatua kali.

  Amesema kitendo cha kuoa watoto wakiwa shuleni au hata chini ya miaka 18 ni cha hatari sana hasa ikizingatiwa kuwa watoto wa kike wanakosa fursa ya kuendelea na masomo ikiwa ni pamoja na kupata madhara mbali mbali ya kiafya.

  “Hakuna anepinga tunapishana tu njia za kuhakikisha haki hii ya mtoto wa kike inalindwa, na niwahakikishie hapa kuwa njia hii ya kulipeleka suala hili katika mahakama ya Rufani ni njia bora kabisa kwani maamuzi yake yatasimama na hayatatenguliwa na yeyote” alisema dkt Mwakyembe.

  Waziri Dkt Mwakyembe amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania ( TAWLA) ambao walimtembelea ofisini kwake na kuongelea vitu kadhaa likiwemo suala hilo la serikali kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: TUMEKATA RUFAA ILI KUPATA MAAMUZI KUTOKA CHOMBO CHA JUU YATAKAYOKUWA KAMA SHERIA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top