JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


TIMU ZA OLIMPIKI ZAKABIDHIWA BENDERA, DSTV WAIPA SHAVU.

Share This

 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia Wambura akiwakabidhi wachezaji bendera ya Taifa kwaajili ya kwenda kupeperusha huko Rio De Jeneiro nchini Brazil wanaokwenda kushiriki mashindano Olimpiki.
 Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, Filbert Bayi akizungumza kabla ya kukabidhi bendera na kuwaaga  kwa wanaokwenda katika mashindano ya Olimpiki Rio De Jeneiro nchini Brazil.
Baadhi ya wadau wa michezo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia Wambura  akiwa katika Picha ya Pamoja na washiriki wa mashindano ya Olimpiki wanaoenda nchini Brazil

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia Wambura amewataka washiriki wanaoenda kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya Olimpiki mwaka huu Rio De Jeneiro nchini Brazil kujituma na kuhakikisha wanafanya vizuri ili kurudi na medali, hayo ameyasema wakati wa kukabidhi bendera kwa timu za kuogelea, judo na riadha leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Wambura amesema kuwa wanapokwenda kuiwakilisha waamini kuwa macho na masikio ya watanzania wote yapo kwao kwahiyo wajitahidi kadri ya uwezo wao kuweza kuhakikisha watakapokuwa wanarejea basi waje wakiwa wamevaa medali zao. " Mnakwenda katika mashindano ya Olimpiki na macho yote ya watanzania yapo kwenu tunategemea mkiwa mnarudi basi tutakuja kuwapokea mkiwa na medali zeni kifuani na hilo linawezekana kama mtajituma mkiwa na ari ya ushindi".

Akiwa anawakabidhi bendera hiyo, Wambura amewaasa wanamichezo hao kutumia fursa nyingine ya kujifunza zaidi kwani kama wataenda kukutana na mataifa mengine mbalimbali. Naye moja ya wadhamini wa safaru hiyo kampuni ya Multichoice Africa, imewataka washiriki hao kujituma zaidi kwani watanzania wote watakuwa wanawaangalia kupitia chaneli zao zinazopatikana kwenye kisimbuzi cha DSTV.

Mkurugenzi wa Multichoice Maharage Chande amesema mwaka huu mashindano yote yatakuwa yanakuja moja kwa moja kupitia channeli za Super Sport na itawapa fursa watanzania kuwashuhudia.wawakilishi wao kwenye mashindano hayo makubwa duniani. Mbali na hilo watakapokuwa huko waitangaze nchi yetu kwa vivutio vilivyopo nchini ili kuzidi kupata watalii mbalimbali kutoka.kote duniani hayo yamesemwa na Godfrey Tengeneza mkurugenzi wa utalii nchini.

Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania , Filbert Bayi amesema kuwa kwa mwaka huu washiriki wamekaa kambi katika sehemu tofauti nchini na wengine wakiwa nje ya nchi na hilo.limefanikisha kuweza kujifua vyema ili kuweza kurejesha ushindi nyumbani. Hilal ameweza kuweka kambi nchini Dubai, Magdalena alikuwa nchini Australia. Andrew aliweka kambi chuo cha polisi Moshi na wanariadha waliweka kambi mkoa wa Arusha.

Washiriki kwa upande wa riadha ni Alphonce Simbu, Said Makula l, Fabian Naasi na Sarah Makela. Timu ya kuogelea inawakilishwa na Hilal Hilal na Magdalena Moshi na Judo ni Andrew Mlungu. Huku timu ya kwanza ikitarajiwa kuondoka alfajiri ya leo wakiambatana na daktari wa timu Nasoro Matuzya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad