728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, August 9, 2016

  TASAF YA ILALA YATOA MILIONI 292 KWA KAYA MASKINI


  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kimanga- Darajani, Kata ya Kimanga Manispaa ya Ilala, Chacha Mwenge akiendelea na zoezi la kuhakiki majina ya wanufaika wa mpango wa TASAF katika mtaa wake leo tarehe 09/08/2016 Jijini Dar es Salaam.
   
  Mratibu wa TASAF wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mwaluma Msofe akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wakunusuru kaya masikini muda mfupi kabla ya zoezi la ugawaji wa fedha hizo kuanza katika mitaa 74 ya Manispaa hiyo leo tarehe 09/08/2016 Jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Kimanga- Darajani, Kata ya Kimanga Manispaa ya Ilala wakisubiri zoezi la ugawaji wa fedha kwa kaya masikini kuanza leo tarehe 09/08/2016 Jijini Dar es Salaam.
  Mmoja wa wanufaika wa Mpango wakunusuru kaya masikini, Ayubu Kabeta akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) muda mfupi baada ya kukabidhiwa fedha za kujikimu leo tarehe 09/08/2016 Jijini Dar es Salaam.
  Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO

  Mpango wa kunusuru Kaya masikini (TASAF) wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala umetoa jumla ya shilingi milioni 292 kwa ajili ya kusaidia kaya masikini 6115 za wilaya hiyo.

  Fedha hizo zimetolewa leo Jijini Dar es Saalam na Mratibu wa TASAF wa Halmashauri hiyo, Mwaluma Msofe ambaye amesema kuwa fedha hizo zitagawanywa kwenye mitaa 74 ya Halmashauri hiyo kwa kuwa ndiyo walengwa wa mpango huo.

  Msofe ameongeza kuwa mchakato wa kuwapata wananchi wenye maisha magumu unafanywa na wananchi wenyewe katika mtaa husika ambapo baada ya kuwatambua  wanathibitishwa mbele ya mkutano wa mtaa.

  “Fedha tunazowapatia wananchi hawa zimeanza kuonyesha mafanikio kwa kuwa zimesaidia kaya hizo kuanzisha miradi midogo midogo inayowawezesha kuendeleza maisha yao pia fedha hizo zimesaidia watoto kupata mahitaji muhimu ya shule hivyo kupelekea mahudhurio kuongezeka”, alisema Msofe

  Mratibu huyo amefafanua kuwa kuna aina mbili za ruzuku ambazo ni ruzuku ya msingi ambayo kaya masikini hupewa kwa mtu yeyote anayetambuliwa na mpango huo wakati ruzuku ya masharti hutegemea na aina ya familia.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kimanga- Darajani, Chacha Mwenge amesema kuwa anaendelea na kazi ya kusimamia na kuchambua majina ya wahusika kwa kuwa kuna baadhi ya wananchi waliingizwa katika mpango huo bila kuwa na sifa kutokana na wananchi hao kutoa taarifa za uongo wakati wa utambuzi.

  “Tumegundua kuwa kuna baadhi ya kaya ambazo  zimeingia kwenye mpango huu kimakosa kwahiyo tunaen
  delea kuzitoa, hadi sasa jumla ya kaya 28 za mtaa wetu tumeshaziondoa kwa sababu ya kukosa sifa”, alisema Mwenge.

  Naye mmoja wa wananchi wanaonufaika na mpango huo, Ayubu Kabeta ameishukuru Serikali kwa kuwapatia fedha za kujikimu pia ameiomba kuongeza kiwango cha fedha hizo kwa kuwa kiasi ni kidogo bado hakikidhi huduma muhimu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: TASAF YA ILALA YATOA MILIONI 292 KWA KAYA MASKINI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top