728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, August 4, 2016

  TANTRADE YASHIRIKI MAONESHO YA NANE NANE MKOANI LINDI

   
  \Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara(TanTrade) Bw Edwin Rutageruka akipata naelezo kutoka kwa Bw John Julius juu ya uzalishaji wa mafuta ya ufuta katika banda la halmashauri ya Masasi kwenye maonesho ya 88 mkoani Lindi. Mafuta ya ufuta yanasoko kubwa sana nje ya Afrika hasa nchi ya Japan na ni mafuta ya pili yenye ubora baada ya olive oil. 

  Lengo kuu tasisi hii kushiriki maonesho haya ni kuunganisha wazalishaji na masoko ya ndani na nje ya nchi. Hivo imekuwa ikipita kwa wazalishaji mbalimbali kuangalia fursa za kuwaungaisha na masoko mbalimbali ili kukuza uchumi wa nchi yetu na pia kualika wawekezaji katika nchi yetu na kuifanya Tanzania yenye viwanda. 

  Tantrade imeshiriki katika maonesho haya maarufu kama 88 kwenye kanda tano ambazo ni Lindi, Morogoro, Mwanza, Mbeya na Arusha na kila mkoa wazalishaji hutofautiana kutokana na aina za uzalishaji wa bidhaa za kila mkoa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: TANTRADE YASHIRIKI MAONESHO YA NANE NANE MKOANI LINDI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top